Friday, June 24, 2022

Mh. Gondwe Afurahishwa na Tamasha la watoto wenye Mahitaji Maalumu lililoandaliwa na Kijiji cha Makumbusho.

Na. Vicent Macha Dsm.

Afisa elimu wa Wilaya ya Kinondoni amepewa siku saba za kuhakikisha Katika shule zote za msingi na sekondari zilizopo katika wilaya ya hiyo kuwepo na walimu walezi.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Godwine Gondwe akiangalia baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na watoto wenye Mahitaji Maalum mapema leo Mkoani Dar es salaam.

Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Mh. Godwine Gondwe katika Tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalum lililoandaliwa na Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Mapema leo mkoani Dar es salaam.

Aidha Mh. Gondwe amesema kuwa ni muhimu sana kuwepo kwa walimu hao mashuleni kwani itasasaidia kuwagundua na kuwapa msaada wa karibu Watoto hao, kwa sababu wanafunzi wanatumia muda mwingi shuleni kuliko majumbani.

Ameendelea kukipongeza Kijiji cha makumbusho kwa kwa kuweza kuandaa tamasha hilo lililojumusha shule mbalimbali za Watoto wenye mahitaji maalum Pamoja na shule za kawaida ili kuwafanya Watoto wachangamane na waweze kucheza na kufurahi kwa Pamoja.

Ameongeza kuwa Watoto wenye ulemavu wanatakiwa,kutambuliwa, kuthaminiwa na kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu ili kuwafanya waweze kuishi katika maisha bora ,huku akikemea jamii kuacha  vitendo vya unyanyapaa kwa Watoto hao.

Katika Tamasha hilo lililobeba kauli mbiu isemayo "Haki Sawa Kwa Wote" limeweza kuwakutanisha wanafunzi kutoka shule za Msingi ikiwemo Mugabe, Uhuru Mchanganyiko, Mikocheni, Makumbusho na Shule ya msingi Jeshi la Wakovu.

Baadhi ya Watoto wenye Ulemavu wakicheza na kuburudika katika Tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalum lililoandaliwa na Kijiji cha Makubusho Mkoani Dar es salaam. 

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Kijiji Cha Makumbusho Bi.Wilhelmina Joseph amesema kwamba Makumbusho ya Taifa itaendelea kuthamini makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo Watoto wenye mahitaji mbalimbali ili kuwafanya wapate haki zao za msingi.

"Tumeandaa tamasha hili ili kuthamini haki za Watoto hawa ,hivyo sisi Kama Makumbusho ya Taifa tumeandaa tamasha hili la Watoto wenye mahitaji Maalumu na tukaweka kauli mbiu ya Haki Sawa kwa Wote" ili kuifanya jamii itambue kuwa hata watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine hivyo wasiwafiche majumbani" amesema Bi Wilhelmina.

No comments: