Wednesday, June 22, 2022

RC MAKALLA: WAKANDARASI WA TAKA, MAWAKALA NA WATUMISHI 19 JIJI LA DSM WATAKIWA KUREJESHA FEDHA BILIONI 10

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla.

Atoa siku 7 kupata maelezo ya kina kwa wote waliotajwa na taarifa ya ukaguzi maalum kuanzia juni 2020/ juni 2021

Fedha zote zirejeshwe ndani ya siku 60 kinyume chake Wote waliotajwa watakabidhiwa TAKUKURU.

Madiwani wamshukuru mkuu wa mkoa kwa maelekezo, wahaidi kuchukua hatua stahiki kwa wote wakiohusika

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa muda wa siku 60 kwa Wakandarasi wa taka, Wakala wa ukusanyaji mapato na Watumishi 19 wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam waliohusika kuchota zaidi ya Shilingi Bilioni 10 za Mapato kuhakikisha wanazirejesha fedha hizo na endapo watakaidi kutekeleza agizo Hilo watafikishwa Mahakamani.

RC Makalla maelekezo hayo wakati wa Kiako Cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambapo pia ametoa muda wa siku Saba kwa Mkurugenzi wa Jiji, Mkaguzi wa ndani, msimamizi wa mfumo wa mapato na Mhasibu kutoa maelezo ya kimaandishi kueleza ni kwanini wameshindwa kudhibiti ubadhirifu wa fedha hizo.

Hatua hiyo imekuja Baada ya Ukaguzi maalumu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG mwaka 2020/2021  kuonyesha kiasi Cha Shilingi Bilioni 10 zilikusanywa lakini hazionekani kwenye mfumo ambapo Wakala wamehusika na upotevu wa Bilioni 4.5 na Watumishi 19 wa Halmashauri kuhusika na upotevu wa Bilioni 5.4 na mpaka Sasa hakuna aliechukuliwa hatua licha ya CAG kuelekeza fedha hizo kurejeshwa.
Aidha RC Makalla ameagiza Baada ya wahusika hao kuhojiwa, Baraza la Madiwani liketi na kupitia upya kasoro zote zilizoonekana na kutoka na maazimio ya kuzitatua.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Mabaraza ya Madiwani  Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kujiridhisha kwa kina Kila taarifa wanazopitisha kwenye vikao Kama ni sahihi.

Hata hivyo RC Makalla pia ameelekeza Halmashauri hiyo kufanyia kazi hoja 18 zilizobaki Kati ya hoja 49 zizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG na kuhakikisha hoja hizo zinafungwa na zisijirudie.

No comments: