Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali(katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wwafanyakazi wa Tigo na wasnii wataopanda leo kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa Nelson Mandela |
Baada ya mafanikio ya ufunguzi wa
msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama
Lote mjini Morogoro, sasa ni zamu ya Sumbawanga na viunga vyake kufurahia
vibe lote katika msimu mkubwa zaidi wa muziki na utamaduni nchini uliowasili
mjini hapo na promosheni tatu kabambe, fursa za kibiashara kwa wakaazi wote
pamoja na ahadi ya vibes moto moto kutoka kwa 100% wasanii wa nyumbani.
Pazia la onesho hilo litakalofanyika
katika viwanja vya Mandela mjini Sumbawanga litafunguliwa na wasaanii
wanaochiopuka waliofanya vizuri katika shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta
2018 – Supa Nyota. Wasanii wa kike Nandy na Maua Sama pia watakuwepo kukongo
nyoyo za mashabiki, wakati wasanii wa hip-hop Fid Q, Bil Nas na kundi la Weusi
linaloundwa na Joh Makini, Niki wa Pili pamoja na G-Nako nao watafunika onesho
hilo. Mashabiki wa muziki pia wategemee kupata vibes za uhakika kutoka kwa
wasanii wa bongo fleva Chegge, Jux, Whozu, Nedy Music, Barnaba na Marioo..
Mdhamini
mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini
Sumbawanga kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kam Lote inawapa wateja hadi mara
mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa
Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo
4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kusini Henry Kinabo alisema.
Tigo
pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa
kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa
mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000
kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia
huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika
kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja
wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila
siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za
mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni
10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya
http://tigofiesta.co.tz
na kuchagua Trivia.
Katibu
Tawala mkoa wa Rukwa, Bernard Makali alielezea
shukrani zake kwa waandaji kutoa fursa ya kuuitangaza wilaya hiyo akisema kuwa
itaibua fursa nyingi zaidi za biashara na kujiongezea kipato kwa wakaazi.
Huu
ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta
2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100%
wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa,
Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na
Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment