Monday, October 30, 2017

WIOMSA - WAZINDUA KONGAMANO LA SIKU NNE LA KUTUNZA NA KULINDA VIUMBE WA BAHARINI

Vitendo vya utililishaji wa maji yenye sumu kwenye bahari pamoja na uvuvi haramu ni hatari kwani usababisha kufa na kutoweka kwa viumbe bahari.
Related image

hayo yamesemwa mapema leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina alipokuwa akizindua kongamano la siku nne la Wanasayansi wa Bahari kutoka ukanda wa magharibi mwa bahari ya Hindi(WIOMSA) akiwa amemuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani.




Waziri Mpina alisema kuwa ni jukumu letu kulinda rasilimali zetu na ndio maana serikali imeweka sera na sheria za kulinda rasilimali hizi adimu na kuchukua hatua kwa wote wanaokiuka sheria hizi, hivyo tusaidiane kwa pamoja kupambana na uvuvi haramu ili kuepusha tatizo la upotevu wa viumbe bahari.

Aliendelea kwa kusema kwamba baadhi ya viumbe bahari vimekuwa vikitoweka kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu.
“Shughuli za Uvuvi haramu,utililishaji wa maji ya sumu kutoka viwandani haya ni mambo makubwa yanayosababisha kupotea kwa viumbe baharini, na ndio maana tumekutana kwenye mkutano huu kujadili ili tuweze kuondokana na tatizo hili”Amesema Mpina.

Aidha katika mkutano huo wadau watajadili mikakati ya namna ya kusaidia kuondokana na changamoto za uvuvi haramu pamoja na matumizi ya kemikali za sumu zinazoingia baharini na kuathiri viumbe hao mfano kemikali hatari ya Zebaki(Mercury).

“Sisi kama serikali tutachukua haya mapendekezo yote yatakayotolewa na wadau hawa ili yaweze kufanyiwa kazi ili kuondokana na hizi changamoto”amesema Mpina.
Kwa wake Mkurugenzi wa wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini, Profesa Yunus Mgaya ameishauri serikali kusimamia sheria zake ili kuweza kudhibiti vitendo haramu vya uvuvi.

“Sheria zipo naishauri serikali itilie mkazo wa nguvu kwenye sheria za uvuvi haramu ambapo itachangia kupunguza vitendo hivi”ameishauri Profesa Mgaya.

Mkutano huo wa siku nne umeanza leo  Octoba 30 na unatarajiwa kumalizika Novemba 4 mwaka huu, ambao umewakutanisha wadau kutoka nchi zaidi ya 30 za mabara yote.
                         
                        

PICHA MPYA YA LISSU INAYOSAMBAA KWA KASI

Ikimuonyesha Mbunge huyo akipata chakula katika Hospital ya Nairobi,

MEYA BWIRE WA MWANZA AWEKWA NDANI BAADA YA KUTAKA KUFICHUA MAOVU YA MKURUGENZI WA JIJI HILO

MEYA wa Jiji la Mwanza, James Bwire amekamatwa na jeshi la Polisi muda mchache kabla ya kutoa salamu zake kwa Rais John Magufuli katika uzinduzi wa kiwanda cha Sayona kwa kuhofia kutoa siri ya ufisadiwa ujenzi wa kiwanda hicho,
Related image
Tukio hilo limetokea baada ya kubainika katika salamu za Meya kwa Rais Magufuli, kulikuwa na maelezo ya ufisadi wa kiwanda hicho kilichopo Nyakato Ilemela jijini Mwanza.
Wanaotajwa kufanya ufisadi huo ni mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kibamba na viongozi wengine wa mkoa huo.
Pia viwanda vya kampuni hiyo vimekuwa vikituhumiwa kuwanyanyasa wafanyakazi wake wengine wakitimuliwa kazi bila kulipwa stahiki zao.
Baada ya kamati ya Ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza chini ya John Mongella kubaini kwamba Meya huyo anataka kumwaga ukweli mbele ya rais, inadaiwa aliliagiza jeshi la Polisi kumkamata kiongozi huyo ambaye kwa kipindi kifupi ameonekana akifichua uchafu unaofanyika katika jiji la Mwanza.

NYARANDO AJIUZURU RASMI UBUNGE WAKE NA NAFASI YAKE NDANI YA CCM, NA HIKI NDICHO ALICHOKISEMA KUHUSU CHADEMA

Aliyekuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne  Mh. Lazaro Nyarando ameamua kujiudhuru rasmi nafasi yake ndani ya chama cha mapinduzi na ubunge katika jimbo lake.
Image result for NYALANDU
Waziri huyo mstaafu amesema kuwa ameamua kuchua hatua hiyo baada ya kuona baadhi ya mambo ndani ya chama hicho hayaendi vizuri, hivyo kuandika posti hiyo katika akaunti zake za mitandao ya kijamii na hiki ndicho alichokisema.

NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.

 HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA,  kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.

VILEVILE, nimemua kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania.


Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. 

Upendo, amani na mshikamano  wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI.

#MunguIbarikiTanzan
ia.
Lazaro S. Nyalandu

Sunday, October 29, 2017

Soma Hotuba ya kusisimua ya Zitto kabwe,Leo kwenye Kampeni Kijichi Dar es salaam

Uchumi wa Nchi Unaanguka, Katiba ya Nchi Inakanyagwa, Utumieni Uchaguzi Huu Kuionyesha Serikali Mnayakataa Mambo Haya.

[Sehemu ya Hotuba ya Kiongozi wa Chama katika Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani - Kijichi]

Ndugu Watanzania
Ndugu Wanatemeke
Ndugu Wanakijichi

Pamoja na masuala haya ya uchaguzi mdogo hapa Kijichi ninaomba nizungumzie masuala machache ya kitaifa. Nafanya hivi kwa sababu baada ya siku thelathini kutoka leo hatutakuwa tena na nafasi ya kuzungumza majukwaani kama viongozi wa vyama vya siasa kwa sababu ya zuio lisilo la kikatiba ambalo limewekwa na Rais dhidi ya mikutano ya hadhara. Hivyo, sisi tumeamua kutumia majukwaa haya ya kampeni za uchaguzi mdogo kuzungumzia mambo ya kitaifa pia.

Tutaitumia mikutano hii ya kampeni kuelezea hali mbaya ya uchumi wa nchi yetu, pamoja na kuminywa kwa haki za wananchi na kusiginwa kwa Katiba ya Taifa letu.

Haki: Nitaanza na hili la haki za wananchi, nyie mtakuwa mashahidi juu ya jambo hili la kuvunjwa kwa haki za wananchi, kwa sababu ya muda nitatoa mifano minne kama ifuatavyo: 

1. Utawala huu wa awamu ya 5 ndio utawala unaovunja haki za watu kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijawahi kuonekana nchini, ndani ya muda wake mfupi wa miaka miwili ya utawala huu, magazeti zaidi ya matatu yameshafungiwa sasa, magazeti yote hayo yalionekana kuwa mwiba kwa Serikali kwa kuhoji na kuandika mambo mbalimbali juu ya hali ya Nchi yetu. Si hilo tu, bado kuna zuio lisilo la kikatiba la Rais juu ya mikutano ya hadhara, huku mamia ya watu wakiwa wameshtakiwa, na wengine kuhukumiwa vifungo na faini, kwa kutumia sheria mbaya ya mitandao ya mitandao ya kijamii, kwa sababu tu ya kutoa maoni yao ambayo yako kinyume na Serikali. Yote haya ni rekodi mpya ya uvunjivu wa haki za wananchi nchini mnayopaswa kuikataa.

2. Ni ndani ya kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya 5, ndipo utu umekosekana kabisa nchini, wananchi wanavunjiwa nyumba zao walizozijenga kwa jasho lao bila hata kulipwa fidia, huku hata mahakama zetu pamoja na Katiba ya nchi kutokuheshimiwa kwa Serikali kuvunja hata nyumba ambazo mahakama imeweka zuio, nyie Wanakijichi ni mashuhuda wa hili, ndugu zenu wa Kimara wamedhalilishwa kwa kuvunjiwa nyumba zao bila fidia na kurudishwa kwenye umasikini. Hali hiyo si Dar tu hapa, wananchi wanavunjiwa nyumba zao bila fidia mikoa mbalimbali nchini, hivi karibuni ni Tabora. Mnao wajibu wa kuwafuta machozi hawa, kwa kuhakikisha mnakikataa chama tawala.

3. Ni kipindi hiki pia ndio tumeshuhudia watu wanaouwawa hovyo hovyo hovyo tu, nanyi ni mashahidi hapa Dar, kila siku inaokototwa miili tu ya watu kule ufukweni Coco Beach, wakiwa wameuawa. Serikali haijawahi kusema chochote juu ya miili hiyo inayookotwa, tuna serikali isiyojali uhai wa watu wake. Si hilo tu, mbunge mwenzangu Tundu Lissu amepigwa risasi zaidi ya 30 zaidi ya mwezi mmoja sasa, mmesikia mtu yoyote amekamatwa kwa tukio hilo? Na msidhani wanaoathirika ni watu wa Upinzani tu, la hasha, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kasulu amepotea tangu mwezi julai, mama mpaka leo hajapatikana. Kuinyima kura CCM ni kuonyesha uhai wa hawa watu una maana kwenu, ni kuonyesha mnajali.

4. Serikali hii imekataa kuwapa haki yenu ya kuwa na mchakato mpya wa Katiba Mpya, mchakato utakaoanzia kwenye maoni ya Tume ya Jaji Warioba, maoni yenu wananchi. Rais anasema kwa kiburi kuwa hakuwaahidi Katiba, na wapambe wake wanazunguka huku na huku kupinga uwepo wa mchakato wa Katiba mpya. Kukikataa chama tawala kwenye uchaguzi huu ni kukiambia kuwa mamlaka ya uongozi ni yenu nyie wananchi, na kwamba mnataka mchakato wenu wa Katiba uendelee.

Hiyo ni mifano michache tu ya ubinywaji wa haki kinyume kabisa na Katiba ya nchi yetu, Katiba ambayo Rais aliapa kuilinda. Wananchi wa Kijichi hampaswi kumchagua mtu atokanaye na chama tawala, chama kinachovunja Katiba na kuminya haki za wananchi namna hiyo kama tulivyoonyesha.

Uchumi: Hali ya uchumi wa Nchi ni mbaya sana, ni mbaya mno kinyume kabisa na takwimu zinazotolewa na kuonyesha kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kuwa kubwa kwa kiwango cha 7%. Mie ni mchumi, pamoja na wachumi wengi wenzangu tunajua kuwa shughuli za uchumi zimedorora, na nyie wananchi ni mashahidi juu ya hali mbaya ya uchumi wa nchi, hili ni jambo la dhahiri kabisa. 

Oktoba 10, 2017 Serikali yenyewe kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ilitoa taarifa yake juu ya hali ya uchumi wa nchi yetu, taarifa iliyoonyesha kuwa hali ya uchumi wa nchi si nzuri kabisa, kukiwa na dalili zote za uchumi wa nchi yetu kusinyaa na kudidimia, mfumuko wa bei ukionyesha kupanda na thamani ya shilingi kudidimia.

Taarifa hiyo inaonyesha namna hali ya uchumi wetu inavyozidi kuwa mbaya zaidi kwa wananchi wa hali ya chini, mfumuko wa bei umepanda mno tangu kuanza kwa utekelezaji wa bajeti ya 2017/18, ongezeko ambalo limechangiwa zaidi na kupanda kwa bei ya bidhaa za chakula (bidhaa ambazo wananchi wengi zaidi mnazitumia).

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia ongezeko hilo ni dagaa asilimia 7.6, matunda makavu kama nazi kwa (3.1), viazi vitamu kwa (3.0), mchele (1.5) na ndizi (1.5). Bidhaa nyingine zilizochangia ni mkaa kwa asilimia 4.0, dizeli (2.4) na petroli (0.6). Ukizitazama bidhaa zote hizi ni zile ambazo zinatumiwa zaidi na wananchi wa kawaida kabisa, nyie watu wa Kijichi. CCM wameamua kuwadumbukiza kwenye umasikini.

Pamoja na kupanda kwa bei za vyakula, taarifa ile ilionyesha kuwa thamani ya sarafu ya Tanzania imeshuka, uwezo wa Tsh. 100 kununua bidhaa umeshuka hadi Tsh. 92.18. Maana yake ni kuwa kama mwaka 2016 shilingi 100,000 ilikupa bidhaa za shilingi 100,000. Mwaka huu 2017 shilingi 100,000 inakupa bidhaa za shilingi 92,000. Kwa hiyo ili upate bidhaa za shilingi laki moja inakubidi uongeze shilingi elfu 8 zaidi. Hali hii inawaumiza mno nyie wananchi.

Wakati Rais wa sasa akiingia madarakani bei ya sukari ilikuwa ninshilingi 1800 mpaka 2000, kwa sasa bei ya sukari ni shilingi 2800 hadi 3000. Gharama za maisha yenu zimepanda mno, Serikali hii imeshindwa kabisa kusimamia uchumi wa nchi.

Lakini msidhani ni uchumi wenu tu nyie watu wa chini ndio mbaya, hapana, ni nchi nzima, jana tulitoa taarifa ya uchambuzi wa takwimu za uchumi wa Serikali inayoonyesha kuwa hali ni mbaya nchi nzima, uzalishaji wa viwanda ukishuka kwa 50%, ujazo wa fedha ukishuka kwa 51%, mikopo kwa sekta binafsi ikishuka kwa 23%, mapato ya bidhaa za forodha yakiwa ni shilingi bilioni 300 tu kutoka bilioni 500 iliyotarajiwa.

Sekta ya Kilimo imeshuka mpaka kiwango cha kabla ya Uhuru, kwani kasi ya ukuaji wa sekta ya Kilimo mwaka 2016 ilikuwa 1.6% tu. Wakulima wa Korosho hawajapewa pembejeo, hivyo uzalishaji wa zao linalotuingia mapato ya Kigeni zaidi nchini utashuka msimu huu wa mavuno, Tumbaku (zao la pili Kwa kuingiza Fedha za kigeni) tayari wakulima wanalia, mazao ya choroko na kunde bei imeshuka kwa zaidi ya 500%, Pamba uzalishaji umeshuka Kwa 63% kati ya mwaka 2015 na 2017 (miaka miwili ya utawala wa awamu ya 5), na mauzo Nje ya dhahabu kuanza kushuka na hivyo kupelekea shilingi kushuka thamani na hivyo mfumuko wa bei kupanda Kwa kasi. 

Kiufupi, ukuaji wa pato la taifa umesinyaa katika robo ya pili ya mwaka huu, ikiwa ni - 0.6, ukuaji hasi ukionyesha kusinyaa kwa uchumi. Tunazo dalili zote za kuanguka kwa uchumi wa nchi.

Wanakijichi, mna sababu tena ya kuendelea kukichagua chama kilichowafikisha kwenye hali hiyo? Mnataka uchumi wa nchi ushuke zaidi? Mnataka watu wetu waokotwe zaidi Coco Beach? Mnataka magazeti zaidi yafungiwe? Mnataka bei ya sukari na vyakula vingine ipande zaidi? Kama hamtaki hilo mnao wajibu wa kumpuuza mgombea wa CCM, na kumchagua mgombea wa ACT Wazalendo, ndugu Edgar Mkosamali ili asaidiane nanyi kutatua kero zenu kama alivyojieleza hapa. Mkifanya hivyo mtakuwa pia mmeiambia Serikali irelebishe masuala haya ya Kitaifa.

Ahsanteni kwa kunisikiliza

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo 
Oktoba 29, 2017
Kijichi 
Dar es salaam

Saturday, October 28, 2017

JIJI LA TANGA LAZIZIMA KWA MSIMU WA TIGO FIESTA 2017 USIKU WA IJUMAA HII

Msanii Aslay akitumbuiza mashabiki waliofurika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumamosi.


Msanii mkongwe wa Taarabu Khadija Kopa  na msanii wa bongo fleva, Ben Pol kwa pamoja wakiwa kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga usiku wa kuamkia jumamosi.

RosaRee akiwa katika jukwaa la Tigo Fiesta

Msanii  Zaidi yao akiimba na mashabbiki zake katika Tamasha la Tigo Fiesta Mkoani Tanga.





Msanii wa bongo fleva, Nandy akiwa kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga usiku wa kuamkia jumamosi.

Tigo yachangia katika ukuaji wa teknolojia na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao nchini A+A- PrintEmail

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Simon Karikari (Kulia) akichangia mada wakati wa mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini, ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam, kushoto ni mkurugenzi wa 361 Degrees Mustafa Hassanali.
washiriki wa  mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini wakifurahia jambo , ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Simon Karikari (Kulia) akichangia mada wakati wa mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini, ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam, kushoto ni mkurugenzi wa 361 Degrees Mustafa Hassanali.


Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Simon Karikari akifurahi jambo na mmoja wa washiriki wa mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini, ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kigwangalla atembelea pori tengefu la Loliondo ashuhudia uhalisia wa mgogoro

Dkt. Kigwangalla atembelea pori tengefu la Loliondo ashuhudia uhalisia wa mgogoro Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla mapema jana Oktoba 27,2017 ameweza kutembelea eneo la pori tengefu la Loliondo lililopo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha na kujionea mambo mbalimbali juu ya mgogoro wa muda mrefu maarufu Loliondo. 

Waziri Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea katika eneo hilo katika kushuhudia kiini hicho cha mgogoro uliozidi zaidi ya miaka 20, ambapo anatarajia kurejesha majibu kwa Waziri Mkuu pamoja na Rais mara tu baada ya kumaliza ziara yake hiyo pamoja na kukutana na watalaam wake wa Wizara. Waziri Dkt. Kigwangalla ameweza kuoneshwa eneo lenye mgogoro baina ya mwekezaji pamoja na wananchi wa jamii ya wafugaji kwenye eneo hilo sambamba na kufuatilia mipaka baina ya maeneo mbalimbali yanayozunguka mipaka ya pori hilo tengefu pamoja na hifadhi ya Serengeti. 

Awali Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika mkutano wa wazi kwenye Mji wa Wasso aliweza kusitisha operesheni zilizokuwa zinaendelea katika pori hilo tengefu la Loliondo na huku akiagiza mifugo yote iliyoshikiriwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo haijafikishwa mahakamani kuachiwa huru huku ile mingine iliyofunguliwa kesi kuendelea kushikiriwa mpaka shahuri la msingi litakapotatuliwa. 

Aidha, Waziri Dkt. Kigwangalla amewataka wananchi hao jamii ya wafugaji katika mgogoro huo kuacha mara moja kuingiza mifugo ndani ya hifadhi licha ya kusitisha Operesheni iliyokuwa ikifanyika na kuwataka wakae meza moja ya majadiriano kupata ufumbuzi. Akiwa ndani ya pori hilo pia alishuhudia kundi kubwa la wanyama mbalimbali kwenye maeneo hayo ambapo imeelezwa awali hawakuwapo kutokana na kukimbia mifugo iliyokuwa imeingizwa na wafugaji hao.
Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla akiwasili eneo la Loliondo kushuhudia kiini cha mgogoro huo
Dkt.Kigwangalla akiwa pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu Mh.Ole Nasha wakati alipofika kukagua kiini cha mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akitazama wanyama eneo lenye mgogoro ambalo ni pori tengefu la Loliondo ambalo awali lilikuwa limevamiwa pamoja na mifugo ya wananchi.
Dkt. Kigwangalla akifuatilia ramani yenye kuonesha eneo la pori tengefu la Loliondo
Baadhi ya wanyama walioonekana wakati Waziri Dkt.Kigwangalla alipotembelea pori hilo ambapo awali wanyama hao walitoweka kutokana na kuingizwa kwamifugo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka (kulia) pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Serengeti William Mwakilema wakati wakikagua maeneo hayo yenye mgogoro huo wa Loliondo.
Dkt.Kigwangalla wakikatisha katika maeneo hayo ya Loliondo wakati akikagua maeneo yenye migogoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akimsikiliza mmoja wa wananchi waliokuwa wakitoa kilio chao kuhusiana na mgogoro huo wa Loliondo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akizungumza na wananchi jamii ya wafugaji (Hawapo pichaani) wakati alipotembelea eneo la Loliondo ili kubaini kiini cha mgogoro huo.

TASNIA HALISI WHATSAAP GROUP YAZINDULIWA KWA KISHINDO JIJINI DAR ES SALAAM


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAANDISHI wa habari ambao ni wanachama wa kundi la Whatsaap lijulikanalo kama TASNIA HALISI wamezindua kundi hilo leo Oktoba 28, 2017 kwa sherehe kabambe ya kukata na shoka iliyohanikizwa na nyama choma, vinywaji vya kila aina na muziki.
Mratibu wa shughuli hiyo, Bi. Angela Msangi amesema, kundi hilo ni mukusanyiko wa wanataaluma na wadau wa habari na linalenga kuwaleta pamoja wana tasnia kwa nia ya kubadilishana taarifa na kusaidiana kitaaluma na kijamii.
Katika uzinduzi huo uliosindikizwa na burudani ya muziki umeshuhudia waandishi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakishiriki.
Katika sherehe hiyo, shampeni mbili zilifunguliwa ikiwa ni pamoja na kukata keki.