Monday, October 30, 2017

WIOMSA - WAZINDUA KONGAMANO LA SIKU NNE LA KUTUNZA NA KULINDA VIUMBE WA BAHARINI

Vitendo vya utililishaji wa maji yenye sumu kwenye bahari pamoja na uvuvi haramu ni hatari kwani usababisha kufa na kutoweka kwa viumbe bahari.
Related image

hayo yamesemwa mapema leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina alipokuwa akizindua kongamano la siku nne la Wanasayansi wa Bahari kutoka ukanda wa magharibi mwa bahari ya Hindi(WIOMSA) akiwa amemuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani.




Waziri Mpina alisema kuwa ni jukumu letu kulinda rasilimali zetu na ndio maana serikali imeweka sera na sheria za kulinda rasilimali hizi adimu na kuchukua hatua kwa wote wanaokiuka sheria hizi, hivyo tusaidiane kwa pamoja kupambana na uvuvi haramu ili kuepusha tatizo la upotevu wa viumbe bahari.

Aliendelea kwa kusema kwamba baadhi ya viumbe bahari vimekuwa vikitoweka kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu.
“Shughuli za Uvuvi haramu,utililishaji wa maji ya sumu kutoka viwandani haya ni mambo makubwa yanayosababisha kupotea kwa viumbe baharini, na ndio maana tumekutana kwenye mkutano huu kujadili ili tuweze kuondokana na tatizo hili”Amesema Mpina.

Aidha katika mkutano huo wadau watajadili mikakati ya namna ya kusaidia kuondokana na changamoto za uvuvi haramu pamoja na matumizi ya kemikali za sumu zinazoingia baharini na kuathiri viumbe hao mfano kemikali hatari ya Zebaki(Mercury).

“Sisi kama serikali tutachukua haya mapendekezo yote yatakayotolewa na wadau hawa ili yaweze kufanyiwa kazi ili kuondokana na hizi changamoto”amesema Mpina.
Kwa wake Mkurugenzi wa wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini, Profesa Yunus Mgaya ameishauri serikali kusimamia sheria zake ili kuweza kudhibiti vitendo haramu vya uvuvi.

“Sheria zipo naishauri serikali itilie mkazo wa nguvu kwenye sheria za uvuvi haramu ambapo itachangia kupunguza vitendo hivi”ameishauri Profesa Mgaya.

Mkutano huo wa siku nne umeanza leo  Octoba 30 na unatarajiwa kumalizika Novemba 4 mwaka huu, ambao umewakutanisha wadau kutoka nchi zaidi ya 30 za mabara yote.
                         
                        

No comments: