Wednesday, October 3, 2012

Rostam Wainogesha IOKOTE ya Maua Sama kwenye Jukwaa la Tigo Fiesta Moshi

ROSTAM- Roma na Stamina wakifanya Maajabu kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote Moshi.

Staa wa Huendi Mbunguni WhoZu akiwapeleka Mbinguni wakazi wa Mji wa Moshi kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote.

Maua Sama alipata nafasi ya kutoa Burudani ya Kutoka kwa watu wake wa Nyumbani Moshi kwenye Tamasha la Tigo Fiesta

Richard Mavoko - Richie Mavoko akiwapagawisha wakazi wa Moshi kwenye Tamasha la Tigo Fiesta

Kundi la WEUSI wakitoa Burudani kwenye Jukwaa la Tigo Fiesta Mjini Moshi

Msanii Rapa Rosa Ree akiimba kwa staili ya kufokafoka kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia jana.

Msanii Nandy akionesha jinsi gani anaweza kuteka mashabiki kwa namna alivyokuwa anaimba nao kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi usiku wa kuamkia Jana.
Kundi la Rostam linalowashirikisha wasanii wawili Roma na Stamina jana walipanda jukwaani kuimba pamoja na msanii Maua Sama wimbo unaotamba kwa sasa ujulikanao kama IOKOTE kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi. 

Tukio hilo liliwafanya mashabiki walipuke kwa shangwe kwa namna wasanii wote watatu walivyokuwa wakiiimba kwa pamoja na kufanya kionjo cha aina yake na kwa ubunifu mkubwa.
Hii ilitokea kabla Maua hajashuka jukwaani ndipo Rostam walipovamia jukwaa na kuimba wote, Na mara baada ya kuimba wimbo huo, wakamalizia kuimba wimbo mwingine walioshirikishana uitwao Kibamia.

Tamasha hili likiwa limemaliza mkoa wa sita usiku wa kuamkia jana, baada ya kupita mikoa ya Morogoro,Rukwa,Iringa,Songea,Mtwara na Kilimanjaro. 
Wasanii mbalimbali walinogesha tamasha hilo wakiwemo Weusi, Chege, Nandi, Me. Blue,Chin Beez, WhoZu, Rosa Ree, Mavoko na wengine.
Kwa upande wa shindano la kutafuta wasanii wenye vipaji Tigo Fiesta Supa Nyota, msanii anayechipukia, Samson Msweta maarufu kama Samson Classic aliibuka kidedea na atauwakilisha mkoa Kilimanjaro kwenye fainali za Tigo Fiesta Supa Nyota mwaka huu jijini Dar es salaam.

Nao Wadhamini wa Tamasha hilo Kampun ya Tigo, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Bagaka alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz
Tamasha hilo litaendelea jumapili hii kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

No comments: