Friday, October 12, 2012

VPL KUENDELEA KUTIMUA VUMBI KESHO

    

     Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa timu
kumi kupambana kwenye viwanja vitano tofauti katika raundi ya saba ya ligi hiyo
yenye timu 14. Polisi Morogoro itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro wakati mwamuzi wa FIFA, Oden Mbaga atakuwa Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya kuchezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na Oljoro
JKT.

      Jijini Tanga, Simba itakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa
Mkwakwani katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani
akisaidiwa na Godfrey Kihwili na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha. Mechi
nyingine za kesho ni Ruvu Shooting dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa
Mabatini mjini Mlandizi, na Mtibwa Sugar watacheza na Mgambo Shooting kwenye
Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Wakati huo huo, Azam imeomba mechi
zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye uwanja wake wa Azam
Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa.

Nayo Ruvu Shooting imeomba
mechi yake ya ugenini dhidi ya Yanga ya Oktoba 20 mwaka huu ichezwe Uwanja wa
Taifa badala ya Uwanja wa Azam Complex. Maombi hayo yatawasilishwa kwenye kikao
cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa kufanyika kesho (Oktoba 13 mwaka huu)
kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi. Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments: