Monday, October 1, 2012

Mr. Blue amuibua Ali Kiba kwenye Vibe la Tigo Fiesta Tanga

Msanii  Mr Blue akiimba katika jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote 2018 lililofanyika Uwanja wa Mkwakwani Tanga

Mkali wa Nyimbo ya Banana Dogo Janja akiwapagawisha wakazi wa Mkoa wa tanga katika Tamasha kubwa la Tigo Fiesta Vibe Kama lote Lililofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Msanii Ali Kiba akiimba pamoja na Mr Blue katika jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote 2018 lililofanyika Uwanja wa Mkwakwani Tanga


Msanii Maua Sama  akitoa Burudani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote,mkoani Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani

Rastam ambao ni Roma na Stamina Pamoja na mkali wa Iokote Maua sama Wakitoa burudani katika Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote




Msanii Rich Mavoko akionyesha uwezo wake katika Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote mkoani Tanga,

 

Mkali wa HipHop Rosa Ree akitoa Burudani katika Tamasha la Tigo Fiesta Mkoani Tanga

Wasanii Kutoka Kundi la Weusi wakipagawisha wakazi wa Tanga katika Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote mkoani Tanga.

Whozu anayetamba na Nyimbo ya Huendi Mbinguni akitoa Burudani kali katika Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote mkoani Tanga

Msanii Khery Sameer Rajabu maarufu kama Mr. Blue jana alimpandisha msanii Ali Kiba kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Mkwakwani mjini  Tanga kwa kushirikiana nae kwenye wimbo wao uitwao MBOGA SABA . Mr Blue alianza kwa kusema "nataka niwape 'surprise"leo toka kwa ndugu yangu mwenye roho ya pekee aje apande hapa juu awasalimie na niimbe nae,". Ndipo Kiba akapanda na kuulipua uwanja  Mkwakwani kwa mayowe, baada ya kumalizika kwa wimbo huo Kiba alisalimia na kushuka jukwaani kitu ambacho mashabiki walitamani aendelee kuimba lakini hakuwa kwenye orodha.
Kwa upande wa wasanii wengine  Rostam na Maua Sama waliendeleza "Remix" yao ya IOKOTE na kuwapa mashabiki Vibe Lote. Nao kundi la Weusi kushirikiana na Nandy waliweza kuimba pamoja na kukonga nyoyo za mashabiki uwanja wa Mkwakwani.

Tamasha la Tigo Fiesta linaambatana na shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama Tigo Fiesta Supa Nyota na kwa mkoa wa Tanga, msanii Faraji Majimoto aliibuka mshindi atayeiwakilisha mkoa wa Tanga. 


Wadhamini wa Tamasha hilo Kampuni ya Tigo, wamewaletea wateja wao ofa kabambe ya intaneti wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+.

Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz
Tamasha hilo litaendelea ijumaa hii kwenye uwanja wa Kiruma mkoani Mwanza.

No comments: