Monday, February 25, 2013

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KENYA SOMA ULINZI ULIVYOIMARISHWA



Utawala wa mikoa nchini Kenya umeunda mfumo wa kutoa taarifa za uwezekamo wa kuzuka ghasia wakati wa uchaguzi mkuu wiki ijayo.

Maafisa wa usalama wamepelekwa katika baadhi ya maeneo yanayodhaniwa kuwa vitovu vya ghasia mkoani Rift Valley, kuweza kuchunguza na kutoa taarifa kuhusu uwezekano wa kuzuka ghasia.

Taarifa hiyo itatolewa kwa kituo maalum ambacho kimewekwa kwa ajili ya kupokea taarifa hizo mjini Nakuru mji ambao ulikumbwa pakubwa na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008.

Maafisa hao, ambao wamepokea mafunzo katika kufanya upepelezi kuhusu ghasia, watatumia simu zao za mkononi, kuwasiliana na maafisa wao wakuu kupitia kwa laini za dharura za simu.

Kituo cha kupokea data pia kimezinduliwa kuweza kudurusu taarifa zitakazopokelewa katika maeneo ambayo heunda yakakumbwa na ghasia.

Taarifa hiyo itatumiwa polisi kuweza kukabiliana na hali yoyote itakayoibuka kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika tarehe nne.

Wakati huohuo viongozi wa makanisa wamewaomba wakenya kufanya uchaguzi kwa amani. Viongoizi kadhaa wamekuwa wakiwakosoa baadhi ya wagombea wakuu kwa kutia doa matokeo ya uchaguzi kwani hata uchaguzi wenyewe haujafanyika.

Wamesema kuwa hilo ni jambo la kutia wasiwasi kwani huenda likasababisha vurugu.

No comments: