Monday, February 18, 2013

NIMR YAJIPANGA

Tatizo la miundombinu ya maabara na majengo ya kutosha limetajwa kama moja ya changamoto kubwa inayoikumba secta ya utafiti Tanzania jambo linalofanya kutokufanya vizuri sana kwa sector hiyo

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini, (NIMR) dacta JULIUS MASSAGA wakati akifungua semina ya siku tatu inayowahusisha wadau wa maswala ya tafiti na watafiti yenye lengo la kukuza uelewa na kujikumbusha mambo mbalimbali yanayohusiana na sector hiyo

Dacta MASSAGA amesema, pamoja na sector hiyo kuonekana inafanya vizuri ikiwa ni pamoja na watafiti wengi kuongezeka lakini changamoto bado zipo huku akitolea mfano kama ukosefu wa rasilimali fedha, na nyingine kubwa kuwa ni ukosefu wa miundombinu ya majengo na maabara za kutosha huku akisema maabara zilizopo nchini pia hazina vifaa vya kutosha

Katika semina hiyo docta KUSAGA amesema lengo kuu la kuwakutanisha wataalam hao ni kuwapa uelewa na mafunzo ya kazi na maadili na pia kupitia tafiti na kuzipa tafiti vibalI

No comments: