Monday, February 25, 2013

ZUNGU ALONGA

 

Wananchi wametakiwa kuzitumia zahanati na vituo vya afya vilivyopo katika maeneo yao, na kuacha mtindo wa kukimbilia katika hospitali za rufaa na hospitali kubwa hata kwa matatizo madogo, jambo litakalosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kubwa.

 

Hayo yamesemwa na mbunge wa ilala Mh MUSA ZUNGU katika ziara ya siku moja  ya chama cha mapinduzi jimbo la ilala katika hospitali ya amana ya kukagua ufanyaji kazi wa hospitali hiyo na changamoto zake.

 

Mh ZUNGU amesema sababu kubwa inayosababisha msongamano mkubwa wa wagonjwa ni tatizo la wananchi wengi kushindwa kuziamini zahanati zilizopo katika mitaa yao na hivyo kukimbilia katika hospitali za rufaa jambo ambalo amesema sio nzuri na linawapa mzigo mkubwa sana wahudumu wa hospitali hizo

 

Katika ziara hiyo mbunge huyo alishuhudia msongamano mkubwa wa wagonjwa wengi wakiwa ni mama  wajawazito, jambo lililomfanya kutoa ushauri kwa serikali kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili waweze kuzitumia zahanati na vituo vilivyopo katika kata zao na sio kukimbilia katika hospitali kubwa.

 

 

No comments: