Friday, March 1, 2013

Tigo Fiesta 2018 Dodoma, burudani ,mwanzo mwisho

  1. Baadhi ya Wabunge na viongozi wa Serikali wakisakata muziki katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.

  1. Msanii wa muziki wa Hip Hop Fid Q akiwapagawisha mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma.

Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki  Rich Mavoko,  akiwaburudisha  mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na maeneo jirani walioshiriki katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani humo. 

Msanii wa Bongo Flava ambaye ni zao la kundi la Tip Top Connection la jijini Dar es Salaam Dogo Janja au akitoa burudani kwa  mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma.

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Whozu pamoja na madensa wake wakilimiliki vilivyo jukwaa wakati wa alipokuwa  akitoa murudani ya kufunga mwaka kwenye Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa David Zimbihile Wilayani  Muleba Mkoani Kagera.
Msanii Rosalee akifanya yake katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.


-Baadhi ya  Wabunge wapanda jukwaani  kusakata Kwaito, Bolingo

-Bill Nas, Weusi ,  Whozu, Rosaree  waacha historia

Na MWANDISHI WETU

Wabunge na viongozi wa Serikali, jana walikuwa ni sehemu ya burudani ya aina yake  katika Tamasha kubwa la muziki la Tigo  Fiesta 2018, lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.

Tamasha hilo lililofanikiwa kuwavuta mashabiki wa muziki wa bongo fleva kutoka mkoa huo na viunga vyake, lilianza kwa msanii Jay Melody kupanda jukwaani  na kutoa burudani safi ‘iliyobamba’na kutengeneza mazingira safi  kwa waliomfuatia

Baada ya wasanii kadhaa kupanda jukwaani i, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi alipanda jukwaani kuongea mawili matatu kabla ya kuomba kuwekewa muziki wa bolingo ambalo alisakata kwa ustadi kmubwa jambo lililozua shangwe za ktosha.

Wakati Katambi akiendelea kusakata bolingo, baadhi ya wabunge wakiongozwa na mbunge wa Sengerema William  Ngeleja waliomba kuwekewa muziki wa Kwaito ambao waliusakata kwa ufundi mkubwa na kusababisha shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki.

Wasanii  wanaounda kundi la Weusi, Bill Nas, Barnaba, Rosaree ni baadhi ambao wataendelea kukumbukwa na wakazi wa Dodoma kutokana na kutoa burudani safi kwa wakazi hao ambao walionekana kuwa na kiu ya buruidani

Ili kunogesha msimu wa Tigo Fiesta 2018, kampuni ya simu za Simu za mkononi ya Tigo imewaletea promosheni bab-kubwa inayojulikana ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman Madati alisema katika tamasha la Mwanza.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia.  Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia. 

No comments: