Friday, June 21, 2013

DAWA YA MAGUGU KUZINDULIWA KESHO TANGA



 Mkuu wa mkoa wa tanga wa mh CHIKU GALAWA anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  katika uzinduzi wa technologia mpya ya kuzuia magugu ijulikanayo kama komesha kiduha hafla itakayofanyika kijij cha mkuzi wilaya ya muheza mkoani tanga hapo kesho
       Akizungumza na waandishi wa habari jijini dare s salaam leo mkurugenzi wa shirika linalojihusisha na kilimo la TANSEED INTANATIONALLY LIMIED bw ISAKA MASHAURI amesema technologia hiyo itawasaidia wakulima wengi katika kupambana na magugu katika mashamba
        Amesema kuwa Katika technologia hiyo  inatumia mbegu ijilikanayo kama tan 222 imetafitiwa kitaalam kuondoa magugu ya kiduha ambayo hunyonya  maji kwenye mizizi ya mimea, mbegu ambayo amesema kuwa imefanyiwa utafiti nchini Kenya miaka kumi iliyopita
        Aidha amesema mbegu hiyo iliyotafitiwa ina uwezo wa kuvumilia magonjwa mengi ambapo amesema ina uwezo wa kutoa magunia 16 hadi 20 kwa hekari moja
          Katika hatua nyingine bw MASHAURI amesema tatizo la magugu katika kilimo halipo Africa mashariki pekee kwani yapo hata nchi za magharibi ambapo ndipo matatizo hayo yalipoanzia

No comments: