Beki wa
Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya
mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika
kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika
Kusini.
Kocha Kim
Poulsen amesema kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki huyo wa kushoto
amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo ni mshambuliaji
Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini kwenye
hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala ya Julai 4
mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Mechi ya
Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye
jijini Kampala, Uganda.
Wachezaji
wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa
(Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruni
Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa
Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).
Wengine ni
Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), Mwadini Ali
(Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum Abubakar (Azam),
Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Vincent Barnabas (Mtibwa
Sugar).
No comments:
Post a Comment