Sunday, June 2, 2013

MADEREVA WA MALORI WAIJIA JUU SERIKALI NA WAAJIRI,WATAKA AJIRA ZA KUDUMU NA MASLAHI MAZURI.SOMA

MAMIA YA MADEREVA WALIOJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MKUTANO HUO ULIOMALIZIKA MUDA HUU HAPA DAR LIVE DAR ES SALAAM

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MADEREVA WA MALORI YAENDAYO  TANZANIA ( CHAMAMATA) BW CLEMENT MASANJA AKISISITIZA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
       Chama cha madereva wa malori nchini Tanzania (CHAMAMATA) kimeitaka serikali kuwahimiza wamiliki wa malori nchini kuwapa madereva hao mikataba ya ajira ya kudumu tofaouti na ilivyo sasa ambapo imeelezwa zaidi ya nusu ya madereva hao wanafanya kazi bila mkataba maalum.
             Akizungumza katika mkutano wa dharura uliowakutanisha madereva wote wa malori nchini na wanachama wote wa chama hicho kwa lengo la kujadili maslahi yao  mwenyekiti wa UMAMATA bw CLEMENT MASANJA amesema madereva sasa wamechoshwa na hali hiyo ya kufanya kazi bila mikataba na wameona ni bora kutoa sauti zao kwa serikali
           
      Bw MASANJA amesema kuwa kutokuwepo kwa mikataba ya kudumu kwa madereva hao kutoka kwa mabosi wao kimesababisha kutokuelewa haki zao kama waajiriwa jambo linalowavunja moyo katika kazi zao
      
        Aidha amesema umefika wakati sasa wa polisi wa usalama barabarani kuanza msako maalumu wa kukagua mikataba ya madereva kama wanavyokagua leseni za udereva na kama watabaini kuna dereva anafanya kazi bila mkataba basi hatua kali ichukuliwe juu ya kampuni husika
        
        Katika hatua nyingine madereva hao kwa umoja wao wameadhimia kukutana na waziri wa uchukuzi dk HARISON MWAKYEMBE pamoja na SUMATRA kwa lengo la kueleza jinsi wanavyonyanyaswa na waajiri wao ikiwemo maslahi duni wanayoyapata.

VIONGOZI WA CHAMAMATA WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO