Imeelezwa kuwa bado zaidi ya nusu ya watanzania wote
hawana uelewa sahihi juu ya ugojwa wa ukimwi jambo ambalo limetajwa kuwa ni hatari katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Hayo
yamesemwa leo jijini dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa tume ya kudhibiti
ukimwi tanzania (TACAIDS)
DK
FATUMA MRISHO
katika mkutano uliowakutanisha viongozi mbali mbali wa afika wanaoshiriki
katika mapambano dhidi ya ukimwi kwa lengo la kuwasilisha taarifa inayohusu
jitihada zinazofanywa na bunge la tanzania katika kupambana na ugonjwa huo
Dk
FATUMA
amesema kuwa katika utafiti uliofanya na tume hiyo katika miko ya tanzania bara
imeonyesha wazi kuwa bado uelewa wa maambukizi ya ukimwi hasa maambukizi mapya
bado ni mdogo jambo ambalo bado linahitaji jitihada za ziada kutoka kwa wadau
mablimbali
Aidha
amesema yapo maneno yanayoenezwa watu
kuwa elimu ya ukimwi imeenea tanzania nzima hivyo hakuna haja ya serikali
kuwekeza nguvu nyingi tena katika kutoa elimu ya ugonjwa huo jambo ambalo amesema
sio sahihi kwani bado elimu ya ukimwi inahitajika sana hasa vijijini ambako
elimu hiyo haijafika vya kutosha.
Katikia
hatua nyingine amesema tanzania ndio nchi ambayo imefanikiwa sana katika
kupambana na ugonjwa huo ambapo amesema kuwa zaidi ya asilimia 93 bado hawana
maambukizi ya ukimwi
Katika
mkutano huo umehudhuriwa na maraisi wastaafu wa afrika akiwemo raisi wa awamu
ya tatu wa tanzania mh BENJAMINI MKAPA
pamoja na raisi mstaafu wa Botswana mh FESTUS MOGAE.
No comments:
Post a Comment