Jaji
mkuu wa tanzania jaji OTHUMAN CHANDE
amesema serikali katika mwaka ujao wa
fedha ipo katika mpango wa kuongeza mahakama kuu nyingine sita katika mikoa ambayo haina
mahakama kuu kwa lengo la kupunguza upungufu wa mahakama tanzania
Kauli
hiyo ameitoa leo katika sherehe za 48 za kuwakubalia na kuwasajili mawakili
wapya 127 leo jijini dar es salaam,amesema
kuwa pamoja na kuwaapisha mawakili hao bado tanzania ina upungufu mkubwa wa
mawakili ambapo amesema tanzania nzima ina mawakili 3455 ambao amesema
ni idadi ndogo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo
Aidha
amesema kuwa mawakili waliosajiliwa leo waende kufanya kazi hasa maeneo ya
vijijini tofauti na sasa ambapo asilimia 75 ya mawakili
wote wapo jijini dare s salaam.
Hata
hivyo amesema kuwa moja ya mjukumu ya majaji hao ni kutenda haki kwa wananchi
wote kama taaluma yao inavyohitaji hivyo amewaasa mawakili hao kuhakikisha
wanazingatia hilo
Katika
hatua nyingine moja kati ya mawakili waliosajiliwa leo bi KONSOLATA
MPEPO
amesema wao kama majaji jukumu lao ni kuwasaidia wananchi katika maswala ya
sheria hivyo amehidi kufanya kazi katika eneo lolote la tanzania
No comments:
Post a Comment