Saturday, July 27, 2013

MTANZANIA AZINDUA KITABU CHAKE CHA MASHAIRI KWA AJILI YA SHULE ZETU,WATANZANIA WATAKIWA KUMPA USHIRIKIANO,MENGI NAYE APONDA MFUMO WA ELIMU TANZANIA

                    C.E.O WA CAMARA EDUCATION TANZANIA AMBAYO NI TAASISI INAYOJISHUGHULISHA NA UTOAJI WA MAFUNZO YA ICT,KUTOA PIA VIFAA VYA COMPUTER,NA PIA OFFLINE WIKIPEDIA ANAITWA EDNA HOGAN AMBAYE NDIYE ALIYETUNGA KITABU HIKI CHA MASHAIRI

              BI EDNA ANASEM KUWA DHUMUNI LAKE KUBWA LA KUTUNGA MASHAIRI HAYO NA KUYASAMBAZA KATIKA MASHULE NI BAADA YA KUONA WATANZANIA WENGI HAWANA MUAMKO WA KUSOMA VITABU NDIPO ALIPOONA NI BORA AKAANZA KATIKA MASHULE MBALIMBALI HAPA TANZANIA ILI WAWEZE UFAIDI MASHAIRI HAYO

            ANASEMA KUWA HAKUWA NA LENGO LA KUJA KUWA MYUNZI WA MASHAIRI ILA ALIJIKUTA ANAFANYA HIVYO BAADA YA KILA SIKU KATIKA MAISHA YAKE YAKE YA KAWAIDA KUKUTANA NA MAMBO AMBAYO ALIBIDI AWE ANAANDIKA MASHAIRI NA MWISHO WA SIKU KUONA NI BORA AKATOA KITABU HICHO

              DADA HUYO AMBAYE WENGI WAMEMUITA SHUJAA NI MOJA KATI YA MASHUJAA WA TANZANIA KWA SASA KWANI KUTUNGA KITABU CHA MASHAIRI NA KUFANIKIWA KIKIPELEKA MASHULENI SIO KAZI NDOGO.

           ANASEMA KUWA LENGO LAKE NI KUHAKIKISHA KUWA KITABU HICHO KINAFIKA SEHEMU KUBWA YA TANZANIA IKIWEMO VIJIJINI NA SEHEMU NYINGINE,HUKU AKITOA SHUKRANI ZAKE KWA SERIKALI NA WADAU WA ELIMU WALIVYOMPA USHIRIKIANO HADI KUFANIKISHA ADHMA YAKE HIYO

ANATOA WITO KWA VIJANA WA KITANZANIA KUJIJENGEA TAMADUNI YA KUSOMA VITABU KAMA NCHI ZA WENZETU KWANI VITABU VINAELIMISHA SANA NA NI JAMBO NZURI KUSOMA VITABU

PROFESA ULIMWENGU ALIKUWA NI MOJA KATI YA WASOMI WALIOVUTIWA SANA NA KITABU HICHO NA KUJA KUMPA USHIRIKIANO MWANADADA HUYO JANA KATIKA HAFLA FUPI YA UZINDUZI WA KITABU HICHO AMBACHO YEYE AMEKIELEZEA KAMA MTUNZI WAKE BI EDNA NI MTU AMBAYE ANA MOYO WA KUDHUBUTU NA ATAFIKA MBALI KWA JITIHADA ZAKE HIZO ALIZOZIONYESHA


BAADA YA MGENI RASMI KUWASILI KATIKA UKUMBI AMBAO ULIFANYIKA HAFLA HIYO

BW MENGI AKITOA MACHACHE
KATIKA UZINDUZI HUO MH MENGI ALIUTUMIA PIA KUTOA MAONI YAKE JUU YA ELIMU YA TANZANIA N A MWENENDO WAKE KWA SASA AMBAPO MH MENGI ALIONYESHA WASIWASI WAKE KATIKA UTOAJI WA ELIMU YA TANANZANIA,MH MENGI ANASEMA KUWA HAIWEZEKANI ELIMU YA TANZANIA KUWA MWALIMU AKIFELI NDIO ANAWEZA KWENDA KUSOMA UALIMU JAMBO AMBALO AMESEMA KUWA HALIMJENGI MTANZANIA AMA MWANAFUNZI BALI LINASHUSHA ELIMU YA TANZANIA KWA SANA

UZINDUZI RASMI WA KITABU HICHO ULIFANYWA NA MH REGNAD MENGI MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP AMBAPOKWENYE PICHA HAPO ANAONEKANA AKIWA NA C.E.O WA CAMARA EDUCATION TANZANIA WAKINYANYUA KITABU HICHO ISHARA YA UZINDUZI RASMI

KATIKA HAFLA HIYO PIA ULIFANYIKA MCHANGO WA PAPO KWA HAPO ILI KUHAKIKISHA KITABU HICHO KINAFIKA MBALI AMBAPO MH MENGI ALICHANGIA ZAIDI YA MILION 50 NA KUAHIDI KITABU HICHO KIENDE KATIKA SHULE ZAIDI YA 31 ZIKIWEMO ZA MKOANI KILIMANJARO

No comments: