Wednesday, July 10, 2013

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO WATAJWA



 
      Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini imetangaza rasmi taarifa ya uchaguzi wa kuingia kidato cha tano,katika shule za secondary za serikali na vyuo vya ufundi huku taarifa hiyo ikionyesha kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi.
      
          Akitoa taarifa hiyo mbele ya wanahabari naibu waziri wa wizara hiyo mh PHILIPO MULUGO amesema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kusoma masomo ya sayansi ni wengi kuliko wale wa masomo mengine,jambo ambalo amesema ni mkakati wa serikali kuendelea kutilia mkazo masomo hayo ambayo awali yalionekana magumu kwa wanafunzi
   
     Mh MULUGO amesema jumla ya watahiniwa 34599  waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana kutoka tanzania bara waliokuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kudato cha tano na vyuo vya ufundi ni 34482 wakiwemo wavulana 23976 na wasichana 10506.

         Aidha akitaja vigezo vilivyotumika kuwachagua wanafunzi hao kujiunga na kidato cha tano amesema kuuwa mwanafunzi alitakiwa kujaza form maalum SELFORM na kuchagua shule anayotaraja kwenda pamoja na kukidhi ufaulu wa masomo ambayo aliyachagua
QIN-----------------------
       Katika hatua nyingine MULUGO amesema kuwa serikali imebadili mfumo wa muda wa kujiunga kidato cha tano ambapo sasa watakuwa wakijiunga mwezi julai tofaui na zamani huku akiwataka 

          MPENZI MSOMAJI TUNAHANGAIKA KUPATA MAJINA YA WOTE WALIOCHAGULIWA HAPA ILI HADI KUFIKIA JIONI UWE UMEYAPATA

No comments: