BREAKING NEWZZZ----JUKWAA LA KATIBA TANZANIA LAIBUKA,LATOA MAONI JUU YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA,SOMA WALICHOKISEMA MUDA HUU

MWENYEKITI WA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA NDG DEUS KIBAMBA AKIONYESHA RASIMU YA KATIBA ILIYOTOLEWA NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA
      Baada ya kimya cha muda mrefu tangu tume ya mabadiliko ya katiba kutoa rasimu ya katiba mpya jukwaa la katiba nchini tanzania limejitokeza kwa wananchi na kutoa maoni yake juu ya rasimu hiyo ya katiba iliyotolewa kwa ajili ya kujadiliwa na kutengeneza katiba mpya
        
         Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania bw DEUS KIBAMBA amesanza kwa kuipongeza tume inayoongozwa na jaji fosefu warioba kwa kutoa rasimu ya katiiba ambayo amesema ina mwanzo mzuri kwa kuingiza baadhi ya mawazo ya wananchi kama yalivyokuwa yanatolewa wakati wa utoaji maoni.
          
        Akizungumza bw KIBAMBA amesema kuwa mchakato huo sasa umeingiliwa na uvyama jambo ambalo amesema kuwa wamekuwa wakionya tangu mwanzo kuwa mchakato huo uwe wa watanzania wote na sio wa vyama fulani vya siasa.

      Aidha amesema kuwa wamekuwa wakiona hata watumishi wa tume hiyo ya mabadiliko ya katiba wakijaribu kutoa mwelekeo wa mabaraza hayo wakitishiwa na kukemewa na makada wa vyama vya siasa kama vile ilivyofanyika kwa mh alhaji SAIDI MAMMRY akiwa mkoa wa iringa

    Jukwaa la katiba limesema kuwa wameshangazwa na tangazo la katibu wa tume hiyo kutaka maoni ya mabaraza na asasi yapelekwe tume kabla ya 31 AGOST jambo ambalo amesema kuwa sio sahihi kwani rasimu hiyo ilichelewa kutoka na hivyo muda umekuwa mdogo

         Aidha amesema kuwa ili mchakato wa kupata katiba mpya uweze kukamilika kwa ufasaha ni lazima mambo yafuatayo yafanyike
1-KUWE NA TUME HURU TA UCHAGUZI

2-TUME YA MABADILIKO YA KATIBA ISHIRIKIANE NA WADAU WENGINE ZIKIWEMO ASASI ZA KIRAIA KUTOA ELIMU YA URAIA BADALA YA KUFANYA PEKE YAKE KAMA SHERIA INAVYOTAKA.

3-MCHAKATO HUO USIHARAKISHWE ILI MABARAZA YA KATIBA NA BUNGE MAALUM YAFANYE KAZI KWA UFASAHA YAKISHIRIKISHA WANANCHI

 4-DAFTARI LA WAPIGA KURA LIBORESHWE KABLA YA KUPIGWA KWA KURA ZA MAONI

HAPA KIBAMBA AKISISITIZA JAMBO WAKATI WA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM MAPEMA LEO JUMAMOSI

WAANDISHI WA HABARI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.