Friday, August 16, 2013

HAWA NDIO WALIOMSAIDIA MASOGANGE NA WENZAKE KUPITISHA UNGA UWANJA WA NDEGE TANZANIA

WAZIRI WA UCHUKUZI MH HARSON MWAKYEMBE AKIZUNGUMZA NA WANAHARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

          Waziri wa ushukuzi nchini tanzania leo ametoa kile alichokiita ni ushahidi wa jinsi madawa ya kulevya zaidi ya kilo 120 yalivyopitishwa uwanja wa ndege wa tanzania ambayo yalikamatwa nchini africa ya kusini na kuwahusisha wasichana wawili ambao ni AGNESS MASOGANGE NA NA MELISA EDWARD PAMOJA NA KIJANA MMOJA AMBAYE NI NASORO SAID MANGUNGA huku akuwataja wahusika walioshiriki katika mchezo huo mzima 

        Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam mh HARSON MWAKYEMBE amesema kuwa katika mchezo huo wamehusika watu zaidi ya watano wakiwemo maafisa ulinzi wa uwanja huo na wfanyakazi wa uwanja wa ndege ambao amesema kuwa walinaswa na kamera za cctv zilizopo katika uwanja huo

          Amwtaja majina ya wahusika ambao walishiriki katika kuupitisha mzigo huo katika uwanja huo kuwa ni 
1-ZAHORO MOHAMED SULEIMAN ambaye ni mbeba mizigo katika uwanja huo ambaye waziri amesema kuwa siku ya tukio kamera zimemwonyesha akizunguka maeneo ya kuingia mithili ya mtu mwenye wasiwasi mkubwa

2-YUSUFU DANIEL ISSA-ambaye ni mfanyakazi wa uwanja huo ambaye kamera zilimwonyesha kujana huyo akitokea nje ya jengo la abiria na kuingia tena mara kadhaa huku akiongea na simu kitendo ambacho hakiruhusiwi katika maeneo hayo

3-ASKARI CPL ERNEST-ambaye alionekana akirandaranda eneo la uhakiki wa hati za kusafiria kama vile anasubiri kitu fulani

       Aidha amesema baada ya muda walionekana vijana wawili wa kike ambao kwa majina wametambulika kama agness gerad na melisa edward  na kijana mmoja wa kiume wakiingia katika uwanja huo  huku wakiwa wamebeba mabeg 9 yaliyofanana
baada ya hapo kamera zinamwonyesha askari ERNRST akiwa anahangaika sana kuwasaidia abiria mbalimbali kuweka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi kazi ambayo ameema sio yake.aidha mmbebe mizigo ZAHORO MOHAMED anaonekana anaonekana akiwasaidia vijana hao wote kupeleka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi na kisha kuyazungushia mabegi hayo mfuko wa nailoni na kuyapeleka kwenye shirika la ndege la africa ya kusini

         Anaongeza kuwa yule mfanyakazi wa uwanjani hapo YUSUFU DANIEL alimnyanyua mwenzake katika kiti cha kukagua mizigo na kukaa yeye ili aipitishe mizigo ya kina masogange na kisha akaondoka baada ya ile mizigo kupita

          Katika hali isiyo ya kawaida kijana NASORO SAID MANGUNGA aliamua nayeye kuondoka kwenda africa ya kusini safari ambayo hakuwa nayo hapo awali ambapo pia alipita bila tiketi ya siku hiyo ambapo mhakiki wa siku hiyo bw MOHAMED KALUNGWANA hakupaswa kumruhusu.

          MWAKYEMBE amesema kuwa siku hiyo mbwa walichelewa kufika uwanjani hapo jambo ambalo lilifanya kutokaguliwa kwa mizio hiyo ikiwa nje.
HIVYO BASI

           Serikali imeagiza mamlaka ya viwanja vya ndege tanzani kuwafukuza kazi maafisa ulinzi wa uwanja huo ambao ni 
YUSUFU DANIEL
JACKSON MANYON
JULIANA THADEI
MOHAMED KALUNGWANA

           Aidha jeshi la polisi limeagizwa kuwakamata wafanyakazi hao mara moja na kuwaunganisha katika kesi hiyo ikiwa ni pamoja na kumwondoa mara moja askari ERNEST katika uwanja huo na kumchukulia hatua kali za kinidhamu


WANAHARI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI

No comments: