SIKUKUU---POLISI DAR YATANGAZA HALI HATARI KWA WAHALIFU,YAPIGA MARUFUKU DISCO TOTO

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM AKIONYESHA BAADHI YA BASTOLA AMBAZO ZIMEKAMATWA NA JESHI HILO KUELEKEA SIKU YA SIKUKUU
         JESHI LA POLOISI KANDA MAALIM YA DAR ES SALAAM LIMETANGAZA KIAMA NA WAHALIFU AMBAO WATATAKA KUFANYA UHALIFU KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU YA IDD NA KUWAHAKIKISHIA WATANZANIA HASA WAISHIO DAR ES SALAAMUSALAMA WA HALI YA JUU

              AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI MAKAO MAKUU YA POLISI LEO KAMISHNA WA KANDA HIYO SULEMAN KOVA AMESEMA KUWA JESHI HILO KUPITIA VIKOSI VYAKE VYOTE VIMEJIPANGA KILA IDARA KUHAKIKISHA HAKUNA UHALIFU UTAKAO JITOKEZA SIKU HIZO ZA SIKUKUU 

         AIDHA POLISI WAMEPIGA MARUFUKU DISCO TOTO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA KILE WALICHOSEMA KUWA NI HATARI SANA KWA WATOTO AMBAO WATASHIRIKI NA KUWATAKA WAZAZI KUWALINDA WATOTO WAO  ILI WASIENDE KATIKA MAENEO KAMA HAYO

             AMEONGEZA KUWA KATIKA KIPINDI HICHO ULINZI UTAKUWA WA HALI YA JUU HUKU DORIA MBALIMBALI ZIKIPITA KWA MAGARI NA HELCOPTA KILA KONA YA JIJI KUHAKIKISHA KUWA HAKUNA UHARIBIFU WA AINA YOYOTE UTAKAO TOKEA

         AIDHA AMEWATAARIFU WATU AMBAO WATAKUWA WANAENDESHA MAGARI HUKU WAKIWA WAMELEWA KUWA KUTAKUWA NA UKAGUZI MAALUM WA KUWASAKA NA KUHAKIKISHA SHERIA INACHUKUA MKONDO WAKE

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.