Thursday, August 15, 2013

WANANCHI WA KEKO WAMCHOKA MWEKEZAJI,WAMTAKA AWASIKILIZE KUHUSU MITARO,DIWANI AUNGANA NAO,MWANASHERIA WA MANISPAA YA TEMEKE AZUA JAMBO AWAAMBIA KAMA VIPI WAHAME HAPO,AMJIA JUU MWANDISHI WA HABARI HII


MH DIWANI MTAWA WA KEKO AKIONYESHWA HALI HALISI YA ENEO HILO

 Wananchi wanaoishi maeneo ya keko mwanga bp leo wamemvaa mwekezaji wa kampuni moja anayejenga eneo kubwa la kuhifadhia maliri maarufu kama godown kwa kile walichokidai kuwa mwekezaji huyo kwenda kinyume na matakwa yao ikiwemo kuziba mitaro iliyokuwa inasafirisha maji kutoka maeneo ya temeke na kujenga mitaro midogo ambayo wamedai italeta matatizo kipindi cha mvua

wakiwa na mbunge wa keko mh fransis mtawa waliingia kwenye eneo hilo linalojengwa kutaka kujua kile ambacho kinalalamikiwa na wananchi hao ambapo walikuta mwekezaji huyo raia wa india akiwa katika shughuli zake kama kawaida

 Katika ziara hiyo ya kushtukiza ya diwani wa keko alijionea mwenyewe eneo hilo ambalo mwekezaji huyo ameamua kuziba na kufumua mifereji iliyokuwa ipo toka zamani na kuweka yake midogo ambayo tayari ilikuwa haifanyi kazi kutokana na maji kujaa pamoja na matakataka jambo ambalo limefanya maji mengi kutuwama.

 Katika sakata hilo wananchi wameonekana kumtupia lawama zote mwanasheria wa manispaa ya temeke ambaye walimtaja kwa jina moja la bw kado ambaye wamedai kuwa amekuwa akicheza mchezo na mwekezaji huyo hivyo kushindwa kumwamrisha mwekezaji huyo atoe mitaro hiyo na kujenga mikunbwa ambayo itatosha


HALI HALISI HAYA NDIO MAKARAVATI AMBAYO WANANCHI WANATAKA YAONDOKE NA UJENGE=WE MTARO MKUBWA KWANI HAYA HAYAWEZI KUBEBA MAJI MENGI AMBAYO HUPITA HAPO


MSOMAJI HUU NI UKINGO AMBAO UNAELEKEA KUIBOMOA BARABARA YA KUTOKA POSTA KWENDA KURASINI AMBAPO MWEKEZAJI HUYO ANATAKA KUPACHIMBA KWA AJILI YA KUWEKA MTARO WAKE

 Katika sakata hilo mh diwani na wananchi waliamua kumwita mtua anayelalamikiwa sana na wananchi hao ambaye ni mwanasheria wa manispaa ya temeke mbaye alifika eneo hilo huku akiwa hataki kabisa kumwona mwandishi wa habari hii huku  akifoka kuwa waandishi wamefwata nini katika eneo hilo jambo ambalo liliamsha hasira kwa wananchi kuona kama anawadharau waandishi wa habari

HUYU NDIE MWEKEZAJI AKIZUNGUMZA NA MWANASHERIA AMBAYE WANANCHI WAMETUPA LAWAMA ZAO ZOTE KWA KE KUWA AMEKULA NJAMA ZA KUWAHUJUMU

 Mwanasheria huyo aliungana na diwani wa keko kukagua eneo hilo ambapo alionekana kutoyaka kuweka wazi jambo hilo huku akiwataka wananchi hao waame kwa kile alichodai kuwa wapo eneo la bondeni jambo ambalo hata diwani wa keko alionyeshwa kushangazwa nalo na kusema sio sahihi.

MWANASHERIA WA MANISPAA YA TEMEKE AKIANGALIA UKUTA MKUBWA AMBAO UMEJENGWA KATIKATI YA MFEREJI WA MAJI NA KUFANYA MAJI KUSIMAMA BILA MWELEKEO

Tulipomfwata mwekezaji huyo kutaka kujua nini kinaendelea hapo aligoma kabisa kuzungumza na mwandishi wa habari 24 kwa kile alichokisema kuwa hana la kuzungumza tumekuja bila kumtaarifu hivyo hawezi kusema lolote juu ya hilo.aidha wakati akizungumza na diwani alisema kuwa haoni jambo kubwa kwani anachojrenga hapo ni eneo tuu la kuhifadhia magari yake na sio kiwanda hivyo anashangaa watu kumwingilia.

Tetesi kutoka kwa wananchi wamesema kuwa wanataarifa kuwa mwanasheria wa manispaa na mwenyekiti wa mtaa huo wamekuwa wakimruhusu mwekezaji huyo kufanya kile anachokitaka kwa kile walichosema kuwa ni rushwa kubwa/

TUNACHUNGUZA UKWELI WA HILI

No comments: