Thursday, September 12, 2013

YULE MKENYA ALIYEPINGWA YANGA APAJA AJIRA RASMI HUKO JANGWANI

        Club ya yanga leo imetengaza kumwajiri rasmi mkenye PATRICK NAGGI  ambaye hapo awali alizua taharuki baada ya wazee wa club hiyo kumpinga, na watu wengine wawili huku ikisema kuwa LAURENCE MWALUSAKO ataendelea kukaimu nafasi ya katibu mkuu  katibu huyo mpya

           Akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam makam mwenyekiti ndg CLEMENT SANGA amesema kuwa maambuzi hayo yalifikiwa na kikao cha kamati ya utendaji jana jijini dar es salaam.

         Wengine walioajiriwa ni BENO NJOVU ambaye ni mshauri wa maswala ya utawala na fedha pamoja na GEORGE SIMBA MAGANI atakeyefanya  shughuli za masoko

         Sanga amesema kuwa waajiriwa wote hao nafasi zao zitatangazwa rasmi baada ya miezi miwili huku akisisitiza kuwa mwalusako anaendelea kukaimu nafasi ya katibu

No comments: