.

TENGA KUMKABIDHI OFISI MALINZI JUMAMOSIRaisi wa anaemaliza muda wake ndani ya shirikisho la soka nchini "TFF" Leodger Tenga anatarajiwa kumkabidhi ofisi raisi mpya wa shirikisho hilo Jaml Malinzi siku ya jumamosi (novemder 2 mwaka huu)/

Jamal Malinzi amefanikiwa kuchukuwa ofisi ya TFF baada ya kumshinda Athuman Nyamlan katika uchaguzi wa kuwatafuta viongozi wapya wa TFF  hapo jana usiku.

Nyamlani na MAlinzi walikuwa wagombea pekee wa nafasi ya uraisi wa TFF na Malinzi kumbwaga Nyamlani kwa kura 73 dhidi ya  52 ya Nyamlani.

wakati nafasi ya uamakamu uraisi wa TFF ikienda kwa Wallace Karia akiwaangusha Iman Madega na Nassib Ramadhani.

Tenga ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Malinzi na uongozi wake mpya kwa lengo la kuendeleza uongozi wake ulipiishia.

Tenga aliwapongeza wajumbe pamoja na walioshinda na kutaka mshikamano uendelezwe kwa ajili ya kulisaidia shirikisho hilo kuendeleza mpira nchini.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.