WAKATI UFOO SARO AKIWA MUHIMBILI HIVI NDIVYO MAMA YAKE ALIVYOZIKWA

 Mamia ya wakazi wa Kibaha mkoani pwani pamoja na jiji la Dar es Salaam leo walimiminika kwa wingi nyumbani kwa Marehemu Anastazia Saro Kibamba Kibwegere kutoa heshima za mwisho kwa mama wa Mwanahabari Ufoo Saro aliye uwawa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenza wa binti yake huyo ambaye pia alijeruhiwa kwa risasi. 

Kwa mujibu wa ripoti ya madkatari walioufanyia uvchunguzi mwili wa Marehemu, Muuaji ambaye alitambulika kwa jina la Anthery Mushi ambaye nae alijiua baada ya kutekeleza tukio hilo alimpiga risasi tano. 
 Mwili wa marehemu ukiingizwa katika Kanisa la KKKT Mtaa wa Kibwegere Kibamba kwa misa maalum,. Marehemu alikuwa akiimba kwaya ya Usharika huo.
  Mwili wa marehemu ukiwa nyumbani kwake.
 Mwili ukiwa ndani Kanisani
 Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho wakiongozwa na baba mchungaji
  Mkurugenzi wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile akitoa heshima za mwishi. Picha ya juu ni mwana jamii.
 Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho pamoja na wanakwaya wenzake na Marehemu.
  Mtoto wa Ufoo, Alvin Mushi akiwa na masikitiko na majonzi makubwa baada ya kuondokewa na Bibi yake pia baba yake ambaye baada ya kuua naye alijimaliza. Alvin anadaiwa kulelewa na Bibi na Babu.
  Ilikuwa simanzi kubwa kwa Bi Joyce Mhavile boss wa Ufoo Saro.
CREDIT ---MAASINDA BLOG

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.