Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akilakiwa na Afisa Habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi
Kasiga (kulia) wakati alipowasili Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
siku ya Alhamisi Okt 24, 2013. Katikati ni Katibu wa wizara hiyo, Juma
Mswadiku.
Mhe.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akiongea na Maafisa wa Ubalozi, kuwapa salamu kutoka Tanzania na
kuwaeleza mambo mbalimbali yanayoikabili nchini yetu ikiwemo suala la
wahamiaji haramu na jinsi gani serikali inavyokabiliana nalo. Suala
lingine ni kuhusu ajira kwa vijana, juhudi anazofanya kuwaelimisha
vijana jinsi ya kujiajiri wenyewe na pia alizungumuzia sekta binafsi
kama zikifanya vizuri zitasaidia sana maendeleo ya nchi yetu na kutilia
msisitizo suala la michezo mashuleni pia alielezea masuala ya vyombo vya
habari na mchakato wa rasimu ya katiba unavyoendelea hizi sasa
Tanzania. Baada ya maelezo ya Mhe. Waziri kulikuwa na kipindi cha
maswali na majibu na kuchangia hoja mbalimbali kuhusu maendeleo ya nchi
yetu.
Mhe.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula
wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi huo, kutoka kushoto ni
Mwambata wa Jeshi Colonel Adolph Mutta, Afisa Paul Mwafongo, Afisa
Switebert Mkama, Afisa Agnes Lusinde, Afisa Mindi Kasiga, Mhe. Waziri,
Mhe. Balozi aliyesimama nyuma ya Balozi ni Afisa Catherine Kijuu, Mkuu
wa Utawala Mama Lily Munanka, Afisa Suleiman Saleh, Afisa Emmanuel Swere
Alfred na Afisa Abbas Missana.
No comments:
Post a Comment