Tuesday, November 26, 2013

HAYA SASA CHADEMA WAMJIBU ZITO LEO,MNYIKA ASEMA ZITO AACHE UONGO,WASEMA AKIENDELEA KUDANGANYA WATAFANYA MAAMUZI MAGUMU,WAANIKA UKWELI WOTE WA SAKATA LAO,SOMA HAPA KWA UMAKINI UELEWE

JOHN MNYIKA AKITOA UFAFANUZI KWA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Na Karoli Vinsent

            SIKU chache baada ya aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kikushutumu chadema kwa uamuzi wa kumvua uongozi aliokuwa nao ndani ya chama hicho.Chama cha Demokrasia na Maendeleo “chadema” kimeibuka na kumpa ukweli wake.
      
           Ukweli wa chama hicho ulitolewa na Mwanasheria wa Chama hicho,ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISU  pamoja Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama hicho ambaye pia ni mbunge wa jimbo la ubungu JOHN MNYIKA,leo makao makuu ya chama hicho jijini dar es salaam  wakati wakizungumza na wahariri pamoja na wandishi wa habari
     
             Kuhusu sababu ya kumvua uongozi ndani ya chadema ENDELEA HAPO CHINI---------


          
                 Kuhusu hoja ya kumfukuza chadema mwanasheria wa chama hicho Tundu lissu alisema uamuzi waliofanya ulikuwa sahihi na wamefuata kanuni zote za chama kwa mwanachama au kiongozi yeyote anayeenda kinyume na taratibu za chama

        “Sheria zipo wazi na sheria hizi sijatunga mimi wala zitto,sheria hizi ni Chama,kwa kiongozi yeyote au mwanachama akifanya mambo kinyume, kamati kuu ya chadema inanguvu ya kumvua uongozi na ikwezekana hata kumfuta uanachama na kamati kuu ya chadema haijavunja katiba”alisema Lissu

       Vilevile mwanasheria huyo akafafanua kuhusu hatua ambazo chama kinachofanya kwa mda huu baada ya kumati kuu ya chadema kuvua uongozi wa chadema zitto kabwe pamoja na mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho Dk kitilo Mkumbo

      “Kwa sasa chama tayari kimekamilisha utaribu wa kuwapa barua kwa maandishi kama katiba ya chama inavyosema na vilevile chama kimewapa fursa ya siku kumi ili waje kujitetea kwenye tena kwa maandishi juu ya tuhuma zinazowakabili kwenye kamati kuu ya chama na chama kitasikiliza na kutoa maamuzi”alizidi kufafanua LISU

         Aidha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama hicho ambaye pia ni mbunge wa jimbo la ubungu JOHN MNYIKA alisema kama watuhumiwa hawo watadharau maamuzi ya chama kuhusu kuja kujitetea baada ya siku kumi na nne basi chama hicho kitafanya maamuzi magumu
  
        “kama siku kumi na nne zikipita watuhumiwa hao hawatafanya busara kuja kujitetea kwenye kamati kuu ya chadema kwa maandishi kama katiba ya chama inavyosema, basi chadema itafanya maamuzi magumu kwa sasa sitaweza kuzungumzia hatua tutakazochukua”alisema John Mnyika

                 Suala la waraka wa siri
          
        Kuhusu walaka wa siri ambao chadema waliunasa kutoka kwenye kompyuta ya Watuhumiwa hao, ukionyesha mikakati ya kukihujuma chama hicho pamoja viongozi wa chama hicho Mwanasheria wa chadema alifafanua na kukanusha ule walaka uliosambazwa kwenye vyombo vya habari amabapo Zitto kabwe aliusambaza wakati akizungumza na waandishi wa habari juzi jumapili kwenye hoteri ya serena jijini Dar es salaama na kusema walaka huo ni tofauti na tulio tumia kumuhukumu kwenye kamati kuu ya chadema,

          “Kuhusu  walaka unaosambazwa na yeye Zitto Kabwe kwenye vyombo vya habari ni tofauti na ule tuliotumia kumuhukumu kwenye kamati kuu ya chama, na mwenyewe Zitto anafanya uwongo wa hali ya juu ili kupotosha uma umwamini juu ya kile anachokisema”alisema Lissu

          Vilevile,Tundu Lissu alisema ukisoma walaka ambao unasambazwa kwenye vyombo vya habari unaonyesha upungufu wa kiongozi huyo na kusema sababu za uwongo za sisi kumuengua chadema
  “Zitto kabwe amewadanganya watanzania kwa kupia walaka ule nataka niwambie watanzania walaka ule anausambaza nakuonyesha kamati kuu kuwa tumemuengua chadema kutokana na Hesabu za Vyama vya kisiasa”,

“kutokana nayeye kuwania nafasi ya mwenyekiti pamoja na ufisadi anausema yeye.Nataka niwambie wanachadema pamoja na watanzania walaka ambao kamati kuu tumetumia kumuhuku hajazungumzia hivyo vitu na wala havipo kwenye walaka amabao tumemuhuku na sisi tutahuto walaka huo mala baada ya siku kumi na nne kupita”alifafanua Lissu

              Kuhusu hoja ya ukuguzi wa fedha ndani ya chadema

    Kwa upande waukaguzi wa matumizi ya fedha ndani ya chadema,Mwanasheria wa chama hicho alisema anayosema mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto kabwe ni dariri ya uongo anaofanya hivyo kwa makusudi na akatoa ushahidi kwa waandishi wa habari juu ya ukaguzi wa fedha ndani chama

     “ Mwaka 2010 mkaguzi aliniaviandika vyama vyote kisiasa vilipie garama ya ukaguzi wa atakaofanya kwenye vyama vya siasa”
 Barua hiyo ilisomeka kama ifuatavyo “mimi sijapewa ruksa ya kukagua ila sijapewa pesa ya kukagu vyama vya kisias”barua hiyo ilitoka na kwa mkaguzi mkuu wa serikali kwenda kwa vyama vya siasa

        Aidha,Mwanashera huyo wa chadema aliongeza na kusema mwaka jana mwezi semptemba vilipereka hesabu kwa mkaguzi mkuu wa serikali pamoja na msajili wa vyama vya kisiasa
“Mwaka jana mwezi semptemba vyama vitatu vilipereka hesabu kwa msajili wa vyama vya siasa ilonyesha Chama cha wananchi Cuf walipereka hesabu zao”
“Na chama cha Nccr mageuzi pia walipeleka pamoja na sisi Chadema,katika ukaguzi ulionyesha vyama viwili tu ndivyo vilivyofanyiwa ukaguzi ambapo na sisi chadema na Nccr nashamshangaa zito kabwe anasema chadema haijakaguliwa sijui ananini huyu mtu”alijoji Lissu
  
           Katika hatua nyingine Mwanasheria huyo wa Chadema alimshutumu aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kuwa Hajawai kufika kwenye ofisi za chadema tangu achaguliwe kuwa mbunge mwaka 2010 hajawai kufika kwenye ofisi za chama hicho


MWANASHERIA MKUU WA CHAMA HICHO AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI JJINI DAR ES SALAAM LEO

No comments: