Tuesday, November 26, 2013

LOWASA AZIDI KUIPINGA ELIMU YA TANZANIA WAZI WAZI,SOMA ALICHOKISEMA


 Na Karoli Vinsent

       WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), amewaomba wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanaweka ushawishi katika suala la elimu bure na bora ili iwe ajenda ya kwanza katika ilani ijayo ya uchaguzi wa chama hicho.

      Akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kigamboni alipokwenda kukabidhi madawati shule za msingi za kata hiyo, Lowassa alisema kutokana na kuhitaji kuona Watanzania wanapata elimu bora ni muhimu ajenda hiyo ikapendekezwa na kila mwanachama wa CCM.
ENDELEA KUSOMAHAPO CHINI-------

     Lowassa alisema kuwa anaamini kuna siku elimu nchini itatolewa bure kwa kila Mtanzania kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kujenga usawa wa matabaka kwa taifa.
“Wana CCM wenzangu naomba tushawishi suala la elimu bure kwa wanafunzi wote wa shule, tena elimu bora liwe la kwanza katika ilani ijayo ya uchaguzi,” alisema.

       Lowassa alisema kuwa hali ya uchumi kwa sasa imeimarika kutokana na uongozi thabiti wa Rais Jakaya Kikwete ambao umeimarisha miumbombinu.
“Wakati Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa anaingia madarakani, alikuta madeni mengi, serikali yake ikafanya juhudi kulipa na kuanza kukopesheka, Rais Kikwete yeye ameunyanyua uchumi kwa kuimarisha miundombinu na sasa hali ni nzuri kabisa, sasa tuelekeze nguvu katika elimu,” alisema.

      Alisema kuwa kwa wale wanaokubaliana na fikra zake za kutaka elimu bure na bora wanapaswa kujenga hoja katika mitandao na sio kupinga tu.
“Najua wako watakaobisha na kusema sana katika mitandao, lakini mimi nawaomba wabishe kwa hoja na iwe ni mjadala katika mitandao na sio kupinga tu, hiyo haisaidii,” alisema.
Lowassa alisema kuwa hafurahii kuona wanafunzi wanakaa chini wakati uwezo wa kuboresha hali hiyo pamoja na maslahi ya walimu inawezekana.

        Aidha, Lowassa alichangia madawati 100 na kutoa changamoto kwa wadau wengine wa elimu kusaidia zaidi huku akiahidi kuchangia shilingi milioni 10 kwa kikundi cha Vicoba cha kinamama wa Kigamboni.
Huu, si mwanzo kwa  Lowassa kuendeleo kuipinga elimu inayotolewa hapa nchini,amekuwa akifanya hivyo tu pindi anapopewa nafasi ya kuchangia kuhusu elimu,

          Wachambuzi, ya masula ya elimu nchini wanaitazama kauli ya Lowasa kuhusu elimu inatija,kutokana na elimu inayotolewa nchini kutomwandaa mwanafunzi kujiajiri mwenyewe,huku wachambuzi hao wakionyesha kuna kila aina ya dariri vijana wakawa bomu mbeleni kutokana na vyuo vikuu vingi kuzalisha wasomi wengi huku wasomi hao wakingojea kuajiriwa na serikali kuliko kujiajiri mwenyewe,huku uchumi wa Tanzania  kutakaa kutoa ajira,

              Mbali na suala la elimu,wachambuzi hawo wakailahumu serikali ya Ccm kwa kuviua viwanda vya ndani, ambavyo vilikuwa vinatoa ajira kwa vijana wengi ambao wanamaliza shure na kutoka vyuo vikuu mbalimbali,
“Mji wa mrogoro ulikuwa na viwanda vingi sana miaka ya nyuma na viwanda hivi vilikuwa vinachukuwa watu wote kutoka kwenye mikoa mbalimbali kwa mfano hapa Dar miaka ya nyuma ulikuwa umkuti mtu katikati ya wiki yuko nyumbani au vijiweni maana watu wote wanakuwa wanafanya kazi viwandani,lakini leo viwanda vile vyote vimekufa na walioviuwa wanajulikana na wapo kwann hawachukuliwi hatua?”walihoji wachambuzi hawo


No comments: