Wednesday, November 13, 2013

KAMA UNAJUA KUWA HELA NYINGI ZA WATANZANIA ZIMEFICHWA USWIS UMEDANGANYWA,HABARI24 BLOG YABAIN KUNA KISIWA KINA MIHELA KINGI YA WANZANIA



Na Karoli Vinsent

       BAADHI ya Watanzania wameficha mabilioni mengi ya fedha katika visiwa vya Jersey vilivyopo barani Ulaya, kuliko hata mabilioni yaliyobainika kufichwa katika benki mbalimbali nchini Uswisi, Habari 24 limeambiwa.
       ENDELEA KISOMA HAPA----


        Taarifa mpya ambazo blogs hii imezipata kutoka Uingereza zinaeleza kwamba fedha za Watanzania pekee zilizoko katika visiwa hivyo zinakadiriwa kufikia kiasi cha pauni za Uingereza milioni 413 (sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.06).
        Fedha hizo zinatosha kuhudumia bajeti za wizara za Afya, Mifugo na Uvuvi, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Afrika Mashariki kwa mwaka mzima bila ya kuomba fedha kutoka kwa wafadhili na bado ‘chenji’ ikabaki.
       Blogs hii haiwezi kutaja chanzo cha habari hizi kwa vile taarifa hii ilipatikana katika mkutano uliofanyika Uingereza wiki iliyopita chini ya kanuni za Chatham (Chatham Rules) ambazo zinakataza kutaja vyanzo vya habari zilizopatikana kutoka katika mikutano inayotawaliwa na kanuni hizo.
     Kwa mujibu wa taarifa za uhakika zilizopatikana, habari24 limeelezwa kwamba zaidi ya Jersey, kuna fedha nyingine nyingi katika visiwa vingine kama Cayman na Isle of Man ingawa pia kuna fedha zilizohifadhiwa jijini London, mji mkuu wa Uingereza.
       “Kuna watu binafsi ambao wamehifadhi fedha zao. Kuna fedha za kampuni kadhaa na kuna fedha za inayoitwa mifuko ya hisani. Naweza nikashindwa kuwapa majina haswa ya wenye fedha hizo lakini nadhani inawezekana kuwapa majina ya kampuni na mifuko hiyo ya hisani (trusts), kilieleza chanzo hicho.
       Kisiwa hicho ni miongoni mwa nchi zinazopendwa na watu, kampuni au taasisi zinazokwepa kulipa kodi au zinazopata mapato yake kwa njia ya kifisadi kwa vile zinatoza kodi kidogo na zina sheria zinazolinda usiri wa walioweka mali zao.
      Mkutano huo ulielezwa kwamba visiwa hivyo vilivyo chini ya Uingereza lakini vinavyojitawala vyenyewe vimehifadhi kiasi cha pauni bilioni 40 kutoka Afrika na katika hizo, pauni milioni 413 zinatoka Tanzania.
        Visiwa vya Jersey vilijipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania miaka michache iliyopita baada ya kubainika kwamba aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Andrew Chenge, alikuwa na akaunti katika visiwa hivyo ambayo ndiyo iliyotumika kumwekea fedha (dola milioni moja) zinazodaiwa kutokana na mauzo ya rada ya kampuni ya BAE Systems kwa serikali ya Tanzania

No comments: