Friday, November 15, 2013

TAARIFA MUHIMU KUTOKA TANESCO,MGAO WA UMEME WATANGAZWA RASMI

            Shirika la umeme tanzania TANESCO linasikitika kuwatangazia wateja wake wote kwamba kutakuwa na upungufu wa umeme kwenye grid ya taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 november mwaka huu kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika kisiwa cha songo songo wilaya ya kilwa,mkoani lindi unaosababishwa na matengenezo ya kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na kampuni ya pan africa.

       Lengo la matengenezo hayo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.Kutokana na matengeezo hayo mikoa iliyounganishwa katika grid ya taifa itaathirika kwa kukosa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti

        Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa yakikosa umeme.

imetolewa na --BADRA MASOUD
                      MENEJA UHUSIANO

No comments: