Thursday, November 7, 2013

TAARIFA MUHIMU,FAHAMU HOMA YA DENGUE NA JINSI YA KUJIKINGA

                 MATIBABU YA UGONJWA WA DENGUE

hakuna tiba ya ugonjwa huu wala chanjo yake bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa.Iwapo mgonjwa atawahi matibabu kwenye kituo cha huduma za afya,kuna uwezekano mkubwa wa yeye kupona
Endapo mginjwa atachelewa kupatiwa matibabu,anaweza kupoteza maisha

                      NJIA ZA KUJIKINGA NA HOMA YA DENGUE

 Ugonjwa wa dengue unazuilika kwa kufanya yafuatayo-


-Fukia madimbwa ya maji au nyunyuzia dawa ya kuuwa viluwiluwi kwenye madimbwi hayo
-Ondoa karibu na makazi vitu vyote vinavyoweza kuwa mazalio ya mbu kama vile vifuu,vya nazi,makopo,chupa ,na magurudumu ya gari ambayo vinaweza kufanya maji kutuama
-Fyeka nyasi na vichaka vilivyo karibu na makazi yako
-Hakikisha kuwa maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama.
-Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko
-Safisha mitaro na gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama

KUZUIA KUUMWA NA MBU

-Tumia dawa za kufukuzia mbu
-Vaa nguo ndefu
-Tumia chandarua chenye dawa wakati wa kulala mchana au usiku 
-Weka wavu wa kuzuia mbu kwenye madirisha na milango

KUMBUKA 

MATIBABU YA UGONJWA HUU HUTEGEMEA DALILI ALIZONAZO MGONJWA KAMA VILE KUWA NA HOMA,UPUNGUFU WA DAMU AU MAJI

No comments: