Tuesday, November 5, 2013

YAMETIMIAAAA-----SUMAYE ATOA YA MOYONI LEO AMCHANA LOWASA WAZIWAZI ASEMA LOWASA ASHTAKIWE


 
Na Karoli Vinsent

       WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amemlipua waziri mkuu mwenzake  aliyejiuzulu ,Edward Lowassa kuwa anafaa kustakiwa kutokana na kitendo chake cha kutoa Siri za Baraza la Mawaziri.

         Sumaye, alizungumza hayo leo kwenye mkutano na waandishi jijini Dar es Salaam,alisema kitendo cha Lowassa kusema kuwa mawaziri wawili ndio waliounga mkono mchakato wa ujenzi wa mradi wa maji  ziwa Victoria ni kosa na uongo.

       “Nashangaa Leo lowassa anavyosema waliokuwa mawaziri wa awamu ya tatu, mawaziri wawiri tu Kikwete na khatibu pekee ndio waliounga mkono mradi huo wa ziwa victoria ni kosa kwani atakuwa anafichua siri za baraza lawaziri ambapo ni kinyume na sheria”

       “Na  jinsi alivyokuwa  anaapa wakatia anapewa uwaziri alisema  kuwa atazirinda siri za baraza la mawaziri vipi sahivi anaanza kusema hivi”alisema Sumaye

       Vilevile Sumaye alishangaa kitendo cha Edward lowassa anavyojisifia wakati alipokuwa waziri wa maji yeye ni mwanzilishi wa mradi huo wa maji wa ziwa Victoria kuwa ni uongo

       “leo anavyojinadi kuwa yeye ndiye waziri aliyeanzisha suala hilo la mradi huo sio kweli yeye anapoingia na kupewa uwaziri huo wa maji alikukuta mradi huo teyali umeanza na hatakama angepewa mtu wa kawaida tu kama wewe mwandishi ungeweza kufanikisha mradi huo’”alisema Sumaye

       Katika hatua nyingine waziri mkuu huyo mstaafu Fredrick Sumaye alisema chama cha mapinduzi CCM kitaanguka kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutokana ruswa kubwa ilyopo ndani ya chama hicho cha siasa.

        “nawaambieni waandishi wa habari hujuma na rushwa inayotumika na wasaka urais kueleke uchaguzi wa mwaka 2015 ndani ya chama chetu cha CCM ni kubwa sana,kama wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm kama hawata waengua basi chama cha mapinduzi kitaaanguka na kutoka madarakani”alifafanua Sumaye

        Katika hari ya kushangaza Sumaye alikiri kufanyiwa rafu mbaya na kundi la watu wanaosaka urais  na akashindwa kuwataja,

           Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanasema hari ya kisiasa ndani ya chama cha mapinduzi ni mbaya sana kutona na kuwepo kwa makundi wanawania urais 2015 ,hari hiyo ilithibitishwa na mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete ambapo alisema kuwa Chama cha mapinduzi kitaanguka kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutokana na kuwepo kwa rushwa kubwa ndani ya chama hicho inayofanywa na watu wanaosaka urais.

      Makundi hayo ambayo yanatajwa katika kuwania nafasi hizo za urais ndan ya CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 ni Edward lowassa, Samweli Sita, Bernard Membe,January Makamba, Stivini Wassira na wengineo

     Ugunzuzi uliofanywa na blogs hii umebaini kuwepo na hatari kubwa sana ndani ya  chama cha mapinduzi na uenda ikapelekea  kuvunjika chama hicho ,kutokana na siasa za makundi ndani ya chama hicho, na endapo kundi moja likikosa nafasi ya urais uwenda kundi hilo likajitoa kwenye chama cha mapinduzi.

No comments: