Saturday, December 14, 2013

EXCLUSIVE----CCM YAWAJIA JUU MAWAZIRI MIZIGO,NAPE ATOA TAMKO KALI KWA JK LEO,ATAKA WAFUKUZWE MARA MOJA,AWATAJA KWA MAJINA


PICHA NA MAKTABA
NA KAROL VICENT ------ CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Rais Jakaya kikwete kuwatimua malamoja moja  mawaziri mizigo kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na Kuendesha Siasa za umangi meza.


      Hayo yalisemwa na Katibu  wa itikadi na uwenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam,Nape alisema kamati kuu ya chama cha mapinduzi ya CCM imefikia maamuzi ya kumtaka Rais Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri hao kutokana na kutowatumikia wananchi na kuendesha Siasa za Umangi meza  katika wizara zao.
ENDELEA KUSOMA HAPO CHINI--------

     “Kamati kuu ya CCM iliyokaa imemtaka Mwenyekiti wa chama chetu,Rais Jakaya  Kikwete kuwachukulia hatua mawaziri saba mizigo kutokana na kushindwa kuwatumikia wananchi na kuendesha siasa za umangi meza,haya maamuzi hatusemi sisi kama viongozi wa kamati kuu,bali maamuzi hayo yanatokana na vilio vya wananchi”.alisema Nape

Nape,aliwataja Mawaziri hao mizigio kuwa ni profesa Jumanne Maghembe ambaye ni waziri wa Maji,Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Christofa Chiza,Waziri wa elimu na Ufundi Shukuru Kawambwa,Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia,Waziri wa Viwanda na Biashara Abdara kigoda.

      Kuhusu waziri wa kilimo, Chakula na Ushirika christofa Chiza
  Nape,alisema Waziri huyo ameonyesha kushindwa  waziwazi kuongoza wizara hiyo kwa kitendo tangu hawe Waziri wa kilimo, katika kipindi cha miaka mine ya uwongozi wake hajawai kwenda kwenye Bohari ya Chakula ya Taifa iliyoko mkoani Ruvuma.

    “Waziri huyu tangu hawe waziri wa Kilimo hajawai kwenda kwenye ghala la chakula kule mkoani Ruvuma,lakini Ukiangalia katika Safari zake za kwenda nje ni nyingi zaidi kuliko zile ambazo makurima ananufaika,na jambo jingine ni Waziri huyo kushindwa kuvisimamia vyama vya Ushirika ambavyo vimekuwa vikiwaibia wakulima”alizidi kufafanua Nape

     Vilevile Nape akafafanua kuhusu kilio  cha wakulima ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu kukosa mbolea kwa wakati,sababu kuu imetokana na Udhaifu wa uongozi wa Waziri huyo.
  
  Kuhusu Waziri wa elimu na Ufundi Shukuru Kawambwa
       Nape alisema Waziri huyo ameshindwa kuisimamia wizara hiyo, kutokana kuzidi madai ya mshahara walimu  pamoja na madeni na kupandishwa madaraja,
   
    Kuhusu Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia,
        Katibu huyo mwenezi na itikadi alisema,Waziri huyo ameonyesha kushindwa kuongoza Wizara hiyo kutokana na Ufisadi wa Mabilioni ya Fedha zinazopotea kwenye Halmashauri mbalimbali hapa nchini huku watu wanaofanya ufisadi huo wakifumbiwa macho tena wanahamishwa kutoka Halmashauli moja kwenda nyingine.pasibo kuchukuliwa hatua.


No comments: