Friday, December 13, 2013

EXCLUSIVE---WANAWAKE WAWILI WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ZAIDI YA KETE 200 ZIKIWA TUMBONI,NI UWANJA WA NDEGE WA JK NYERERE,WALIKUWA WANAPELEKA CHINA

KAMANDA WA UWANJA WA NDEGE WA JK NYERERE ASP RENATUS CHALYA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO OFISINI KWAKE.

Na karoli Vinsent

        MIEZI michache kupita  Tangu waziri wa uchukuzi dokta Harisoni Mwakyembe kufanya mabadiliko kwenye uwanja wa kimataifa wa Uwanja wa ndege wa Mwalimu JK NYERERE ,watu wa wawili wamekamatwa wakisafirisha madawa ya kuleva.
 ENDELEA HAPO CHINI--------

    Hayo yamethibitiswa leo na kamanda wa Polisi wa  Uwanja wa Ndege wa JK NYERERE Asp Renatusi Chalya,wakati akizungumza na wandishi wa habari.Alithibitisha kukamatwa kwa wanawake wawili ambao walikuwa wakijalibu kusafirisha madawa kutoka Tanzania kwenda China,

     Chalya,amesema wanawake hao walikamatwa jana tarehe 11 majira ya saa kumi na mbili usiku wanawake aliwataja kwa majina kuwa Mariam Hamadi umri wa miaka 29 kabira ni Mhehe, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam ambaye paspoti yake ni Ab,576285,pamoja na mwenzake Khadija Abduli umri miaka 30 kabira ni Mnyamwezi makazi wa Tabata Kisukulu Jijini Dar es Salaam.

       Kamanda Chalya alisema watuhumiwa hao walikuwa  wanataka kusafiri na shirika la ndege la Quatal  ndipo askari waliokuwepo uwanjani walipowatilia shaka Abaria hao ,Na kuanza kuwanawabana pamoja na kuwapekuea ndipo Mariam Hamadi alikubari kuwa amemeza kete 72 za madawa ya kulevya,mpaka mda huu alikuwa ametoa kete 22 kutoka tumboni mwake.

      Katika hali ya kushangaza Mtumiwa wenzake Khadija Abduli alikataa kubeba madawa ya kulevya na kusema  yeye alikuwa anamsindikiza rafiki yake ambae ni Mariam.Katika kuonyesha umakini kwa polisi waliokuwepo uwanjani hapo wakazidi kumbana ndio wakagundua alikuwa na kete 122 na  yeye kuzitoa kete hizo alizokuwa amezimeza tumboni mwake.

     Katika hatua nyingine kamanda wa Polisi wa  Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Juliusi Kambarage Nyelele Asp Renatusi Chalya amesema jana jeshi hilo la polisi,majira ya saa 7 mchana,jehi hilo la uwanjani hapo  limemkamata mtu mmoja mbaye ni Raia wa China, bwana Guyan Juhim mwenye paspoti yenye namba  T609987,ambapo mtu huyu alikamatwa na Madini kilo 82 ambapo alikuwa anayasafilisha kinyume na taratibu.

    Vilevile Kamanda Chalya amewahasa wananchi kwa kuwataka wafanye kazi zingine kuliko biashara chafu za Madawa ya kulevya kwa kuwa hazina tija na wala hazijengi,na kusema kwa sasa jehi hilo la polisi kitengo cha uwanja wa ndege limejipanga kukabiliana na biashara hizo chafu ambazo zimekuwa zikiitia nchi aibu kubwa katika medani za kimataifa





No comments: