Monday, January 27, 2014

BAADA YA MAKUNDI KAMA MBWA MWITU KUSHAMIRI DAR HUU NDIO MKAKATI MPYA WA KUYATOKOMEZA,KOVA ATOA TAMKO,SOMA



KAMISHNA KOVA AKIZUNGUMZA NA WAAMDHISHI WA HABARI LEO
     Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limeanzisha program mahususi ya kuimarisha ulinzi na usalama hadi ngazi za mitaa. 
      Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana ya kuzuia na kudhibiti uhalifu jijini D’Salaam hadi ngazi ya Kata.  Sasa tumeamua kupeleka huduma za ulinzi karibu zaidi na wananchi hadi ngazi za mitaa. 

        Wenyeviti wa Serikali za Mitaa watashirikiana kwa karibu na wakuu wa vituo vya Polisi ambao watawajibika kupanga askari wa vikosi mbali mbali katika kila mtaa ili kuhakikisha kwamba mitaa yote jijini D’Salaam ina ulinzi wa kutosha.  Kila mtaa utapangwa askari katika mtindo wa wenye eneo la doria inayokidhi mahitaji ya usalama (Beat Area), Askari watakaopangwa hapo ni pamoja na askari wa kawaida (GD), askari wa Upelelezi, Askari wa Usalama Barabarani nk. 

       Askari hao watashirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na raia wema wa eneo hilo.  Aidha wadau mbali mbali watasaidiana na Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara na wananchi kwa jumla ili kuhakikisha kwamba kila mtaa jijini D’Salaam unakuwa huru katika suala la uhalifu. 

Program hii inaenda sambamba na dhana ya Polisi Jamii na maboresho yanayoendelea katika Jeshi la Polisi.Kila mwanamtaa ajione kwamba anao wajibu wa kuchangia katika suala la Ulinzi na Usalama katika mtaa wake.   

No comments: