Monday, January 27, 2014

MAJANGA---WAKALA WA KUWATAFUTIA AJIRA WATANZANIA EROLINK NI FEKI,WAITIA ASARA SERIKALI YA BILLION TATU,SOMA HAPA

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA GAUDENSIA KABAKA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
    Wizara ya kazi na ajira leo imetangaza rasmi kuwa kuna mawakala ambao wanawatafutia watu kazi ambao ni feki na wanaitia serikali hasara ya pesa nyingi kitu ambacho wamesema ni janga kwa taifa ambapo wamesitisha mara moja utaratibu huo ili utaratibu ufwate

         Akizungumza na wanandishi wa habari jijini dare s salaam leo waziri wa kazi na ajira mama GAUDENSIA KABAKA amesema kumekuwa na mfumuko wa mawakala wanaojitoa kuwasaiidia vijana kupaja ajira kwa maslai yao huku akiitaja kampuni mja maarufu Tanzania kwa kazi hiyo ambao NI EROLINK TANZANIA ambayo imekuwa ikishutumiwa kwa kuwatesa sana vijana wa kitanzania na kuwatumikisha pasipo haki zao za msingi kama wafanya kazi halali

      Waziri KABAKA amesema kuwa EROLINK ni mawakala feki na hawapo kisheria na tayari wamekwisha iingizia serikali hasara ya bilion tatu kwa miaka mitatu jambo ambalo amesema kuwa lazima walifwatiliie kuona jinsi ya kuwaadhibu watu hao kisheria.

        “Tunawapa mwezi mmoja mawakala hawa waje ofisini kwetu ili wasjisajili kwa mujibu wa sheria kwani tunatambua mchango wao na tunawahitaji sana ila lazima wafanye kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na sio kiwanyanyasa watanzania kwa sababu ajira inekia ngumu”alisema waziri kabaka.

JITIHADA ZA KUWATAFURA WAHUSIKA WA EROLINK KUELEZEA TUHUMA HIZO ZINAENDELEA KAMA UNAHUSIKA TUPIGIE 0712098645


No comments: