Thursday, January 23, 2014

CCM YAGOMA KUMPONGEZA RAISI KWA BARAZA JIPYA

 Na Karoli Vinsent
       
   
         SIKU chache kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete Kuteua na kuapisha Baraza jipya la Mawaziri ,Chama cha Mapinduzi CCM kimeshindwa kupongeza Uteuzi  na Badala yake Chama hicho kimesema Waziri yeyote hasiyeweza kazi aondoke kabla chama hicho hakijamchukulia hatua.
ENDELEA---------

        
    Hayo,yagundulika leo Ofisi Ndogo za chama hicho jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano  na Waandishi uliondaliwa na Katibu mwenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi CCM,Nape Nnauye ambapo alisema  chama hicho kinaamini uteuzi huo umewapa fursa kwa mawaziri mizigo kujirekebisha .
    
      “CCM inaamini kurudishwa kwao Mawaziri hao,ni njia ya kuwapa fursa kujirekebisha kasoro zao mbalimbali.Na pia tunaamini watafanya kazi kwa makini na kwa weredi,Ila Chama cha Mapinduzi tunasema kwa kauli moja,Waziri yeyeyote ambaye anaona hawezi kazi aondoke mwenyewe kabla chama hicho hakijamchukulia hatua”Alisema Nape
         
    Vilivile Nape, alisema Hoja ya kufukuzwa mawaziri mizigo si ya kiongozi yeyote wa Chama hicho ,Bali ni hoja ya wananchi.
      
    “ Nataka niseme Hoja ya kuwafukuza mawaziri kwenye nyazifa zao si hoja ya Nape wala hoja ya katibu wa CCM bali ni hoja ya Wananchi wenyewe ambao wanakumbana na matatizo  mbalimbali ,na hii iliibuka wakati wa Ziara ya kukijenga Chama Mwishoni mwa mwaka jana ambapo tukiwa kwenye ziara hiyo, tumefuatwa na makundi mbalimbali hususani Wakulima,wafugaji,Walimu pamoja na Wasomi  wanalalamika juu ya utendaji  wa mwaziri hao huku wengene wakihoji uharali wa Chama hichi kuwafumbia mawaziri hao huku wakiwa wameshindwa kuwajibika?”
        
    “ Chama hichi ni cha Wakulima na wafugaji na Walalahoi na tunavyopewa malalamiko kama haya lazima tuyafanyie kazi a na sii kuyapuzia na katika mambo ambayo walikuwa wanayapigia kelele ni mawaziri hawa tena wengine wakiwataja kwa majina”alisema Nape
       
    Kitendo cha cha kurudishwa kwa mawaziri mizigo kinatafsiriwa kama Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa, anadaiwa kukisaliti chama chake kwa kuwarejesha mawaziri mizigo ambao hivi karibuni walipendekezwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM kwamba wang’olewe kwa utendaji wao mbovu.

     Ikumbukwe kwamba chimbuko la mawaziri mizigo lilitokana na ziara ya Katibu Mkuu, Abdulhaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi taifa, Nape Nnauye, katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo waliwataja baadhi ya mawaziri kuwa ni mizigo.

      Katika mikutano tofauti ya hadhara, viongozi hao wa juu wa CCM walimtaka Rais Kikwete awatimue mawaziri mizigo kwa madai kuwa walishindwa kuendana na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

       Wakiwa bado ziarani katika mikoa hiyo, Kinana alisema mawaziri mizigo watahojiwa na Kamati Kuu ya CCM na hata baada ya kuwahoji, CC iliyoketi mbele ya Rais Kikwete mjini Dodoma ilipendekeza watimuliwe.

        Mawaziri waliotajwa kuwa mizigo ambao jana waliapishwa na kurejea kwenye nafasi zile zile ni pamoja na Waziri wa Kilimo na Chakula, Christopher Chiza, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

      Lakini baada ya kuwaacha mawaziri mizigo, Rais Kikwete aliwatupa nje mawaziri watano, akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Binilith Satano Mahenge na Naibu wake anakuwaUmmy Ali Mwalimu.

      Katika mabadiliko hayo, pia Rais Kikwete aliwatupia virago manaibu waziri wanne, ambao ni Gregory Teu, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Philip Mulugo, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Goodluck ole Medeye, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict ole Nangor

      WADAU WANENA BAADA YA KAULI NA NAPE KUTOPONGEZA BARAZA LA MAWAZIRI

      Baadhi ya makada maarufu wa chama hicho ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, waliliamwambia mwandishi wa mtandao huu kuwa kitendo cha Rais Kikwete kutomtimua hata waziri mmoja kati ya wale waliopendekezwa na chama chake baada ya kujiridhisha kwamba hawana uwezo kiutendaji, ni usaliti wa hali ya juu na unakiweka chama hicho katika mazingira mabaya.

      “Si tu kwamba amekiweka chama mahali pabaya, bali pia amewashushia hadhi mzee Kinana na Nape ambao wamerejesha imani ya wananchi kwa chama kwa kiwango kikubwa,” alisema kada huyo ambaye pia ni mmoja wa wenyeviti wa CCM wa moja ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

        Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (CC) ya CCM, alisema hata baada ya Kinana na Nape kutaja majina ya mawaziri mizigo na kutaka waitwe kuhojiwa na Kamati Kuu, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao wa chama kuongeza majina mengine ya mawaziri mizigo ili wahojiwe na kuchukuliwa hatua.

       “Katika orodha ya Kinana na Nape, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, hawakuwemo. Hawa waliongezwa baadaye kwa agizo la Rais. Na bado kulikuwa na pendekezo hata la kutaka kumwita na kumhoji Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwamba amezembea kupata fedha za msaada kutoka nje kwa ajili ya kuboresha reli na bandari.

      “Rais kama mwenyekiti ameshiriki kikao cha kuwahoji na amepokea mapendekezo, leo amepuuzia mapendekezo ya chama. Wana CCM watawaangaliaje kina Kinana na Nape? Watawezaje kwenda tena kwenye ziara na kuikosoa serikali yao?” alihoji kada huyo.

          Kiongozi mwingine wa CCM jijini Dar es Salaam, alisema kwa kawaida chama kinachoongoza serikali ndicho chenye nguvu na kinapotoa maoni dhidi ya serikali kiliyoiunda lakini yatekelezwe.

        Kada huyo alikwenda mbali zaidi kwa kumlaumu Rais Kikwete kuwa hata kwenye mchakato wa Katiba kuna uwezekano mkubwa mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuhusu serikali tatu ni tofauti na msimamo anaouzungumza kwenye chama.

        “Warioba na tume yake wamekuja na mapendekezo ya serikali tatu, wanapokutana na rais kujadili maoni hayo, bila shaka wanaimba lugha moja, anapokuja kwenye chama kinachoamini kwenye serikali mbili, anaimba wimbo huo huo. Mwisho wa siku msimamo wake uko wapi? Sitashangaa kuona chama kitaachwa kwenye mataa kama kilivyoachwa kwenye hili la wabunge mizigo,” alisema.

No comments: