Monday, January 27, 2014

KAMISHAMA KOVA AUNGURUMA DAR,NGOZI MBLI ZA CHUI ZAKAMWATWA

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM SULEMAN KOVA AKIONYESHA NGOZI MBLI ZA CHUI AMBAZO ZIMEKAMATWA NA POLISI

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa MWAJUMA D/O HAMIS, Mkazi wa Yombo Vituka kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni ngozi mbili za Chui, thamani yake inakadiriwa kufikia shilingi za kitanzania millioni 11,259,500/=.

    Tukio hili lilitokea tarehe 18/01/2014 huko maeneo ya Yombo Vituka (W) Chang’ombe (M) Temeke baada ya mtoa taarifa ambaye ni Afisa Mhifadhi Wanyama Pori mkazi wa Ukonga kutoa taarifa kituoni hapo kuwa huko maeneo ya Yombo kuna mwananchi anauza ngozi za chui.

   Askari walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa na walipopekua chumbani kwake walikuta nyara hizo. Upelelezi wa shauri hilo unaendelea.


No comments: