Thursday, January 9, 2014

mpyaaa---DK SLAA AZUA JIPYA AIJIA JUU TUME YA UCHAGUZI,SOMA ALICHOKISEMA LEO



       Na Karoli Vinsent
        
     KATIBU mkuu wa  chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ameivaa Tume ya Taifa ya uchaguzi Nchini NEC na kusema inawanyima vijana  fursa katika chaguzi mbalimbali .
ENDELEA HAPO -------

       
        Hayo yalisemwa leo na katibu wa chama hicho DK Wilbrodi Slaa katika semina iliyoandaliwa na Tume ya uchaguzi nchini kwa ajili ya vyama vya kisiasa nchini.Slaa alisema inashangaza kuona mpaka sasa Daftari la kudumu la wapiga kura alijawaandikisha vijana wanaofikia Milioni 2 na nusu.

      “Nidhahili kuwa serikali inawanyima Fursa vijana katika kupiga kura.inashangaza sana Daftari hili la kudumu la wapigakura  alijafanyiwa marekebisho tangu 2007 hebu jiulizeni ni vijana wangapi wamefikisha umri wa miaka 18 tangu kipindi hicho hadi leo ?”alihoji Dk slaa
    
      Dk slaa alizidi kufafanua na kusema Tume ya uchaguzi imeshindwa kufanya majukumu yake,na kuendesha ofisi kwa mazoea kwa kushindwa kununua mitambo mipya.
     
     “Kwanini serikali inashindwa kununua mitambo mipya tena kwa ajili ya kuwasajili vijana wapya katika daftari la wapiga kura,akati leo ukiangalia katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012  inasema kila mwaka vijana wanaofikisha umri wa miaka 18 ni zaid ya miloni 3.sasa hebu jiulizeni tangu mwaka 2007 mpka leo ni vijana wangapi wamenyimwa fursa katika nchi yao iliwaweze kupiga kura”alisema Dk Slaa
     
      Kwa upande,wake mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Profesa Ibrahimu Lipumba kwa upande wake aliitupia lawama tume hiyo kwa kufanya kazi yake kizamani kutokana na mtandao wa Tume hiyo kuonyesha wazi tume hiyo imeshindwa kufanya kazi zake kwa ufasa

      “Ukienda kwenye mtandao wa Tume hii ya uchaguzi utapata taharifa ya uboreshaji wa tume ya uchaguzi ulifanyika 2007,leo tunakuja hapa tunaambiwa tume imefanya kazi kubwa kazi hipi hiyo? kama si kuwadanganya wananchi”alisema Lipumba

No comments: