Thursday, February 20, 2014

POSHO YA BUNGENI NA MIZWENGE YAKE-- SOMA

Huku rasimu ya kanuni za Bunge la Katiba ikitishia kuwanyima posho nono ya Sh 220,000 kwa siku wajumbe watakaoshindwa kuheshimu kiti, baadhi ya wabunge wameanza kunung’unika kiwango hicho walichowekewa “hakikidhi mahitaji.”

Dodoma. Huku rasimu ya kanuni za Bunge la Katiba ikitishia kuwanyima posho nono ya Sh 220,000 kwa siku wajumbe watakaoshindwa kuheshimu kiti, baadhi ya wabunge wameanza kunung’unika kiwango hicho walichowekewa “hakikidhi mahitaji.”

Rasimu hiyo ya kanuni inasisitiza kuwa mjumbe anayeshindwa kufuata taratibu anawezwa kusimamishwa, na hatapokea posho hiyo kwa kipindi chote atakachokuwa benchi.

Hata hivyo, wabunge mbalimbali walisikika leo asubuhi wakisema kuwa kiwango hicho cha Sh 220,000 ni kidogo sana, hali inayofanya washindwe kumudu gharama za maisha mjini Dodoma.

Richard Ndassa (CCM-Sumve) aliiambia Mwananchi kiwango walichowekewa ni sawa na “posho aliyokuwa akilipwa dereva wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.” “Hii siyo sawa kabisa,” alisisitiza.

Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi alikuwa na haya ya kusema: “Sisi tumeshazoea maisha ya Dodoma na tunaishi hivyo hivyo tu licha ya kuwa fedha ni ndogo.”

“Ila hawa wenzetu ambao ni wageni hali zao ni mbaya.”

Katika jitihada za kuzima fukuto hilo la posho, Mwenyekiti wa muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho aliahidi kulirudisha suala hilo serikalini ili litazamwe upya.

via mwananchi

No comments: