Thursday, February 20, 2014

UFAFANUZI KUTOKA MSD


IDARA ya Bohari ya Dawa nchini (MSD) Imekanusha Taaarifa zilizokuwa zimeripotiwa kwenye vyombo vya Habari nchini kuhusu Utata kwenye Manunuzi ya Dawa kutoka Nje,Badala yake imesema inafuata taratibu zote za Mananuzi.
      Hayo,alisema leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa nchini,Cosmas Mwaifano wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo alisema utaratibu wa uagizaji na uingizaji wa Dawa ndani ya nchi huratibiwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Chakura na Dawa.

     “Nataka niwambie ukweli wananchi utaratibu wa uagizaji na uingizaji wa Dawa ndani ya Nchi huratibiwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),kuwa dawa yeyote kabla ya kuingizwa nchini lazima iwe imesajiliwa na Mamlaka na hukaguliwa pindi inapogombolewa ili kuhakikisha ubora wake”amesema Mwaifano

      Aidha Mwaifano amesema taratibu za manunuzi katika bohari kama ilivyo taasisi nyingine  yoyote ya serikali na husimamia na kuongozwa na sheria Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011 na kanuni zake za Mwaka 2013.
  
       Vilevile,Mwaifano amesema njia inayotumia katika manunuzi ya bidhaa ndani ya Bohari hiyo ni kupitia zabuni za kimataifa na hii ni kutokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia 80 ya Bidhaa hutoka nje ya nchi.

No comments: