TAARIFA MUHIMU TOKA TFF.SOMA 


        
        Fomu za wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam zimeanza kutolewa leo (Februari 24 mwaka huu).
         
        Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo zinazotolewa Idara ya Habari (Maelezo) ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.
         
      Ada kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.
   
        Kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(i), sifa ya elimu kwa wanaowania nafasi za Mwenyekiti hadi Katibu Msaidizi ni diploma au digrii ya uandishi wa habari. Kwa nafasi nyingine kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(ii) ni cheti cha ngazi yoyote katika uandishi wa habari.
     
     Tunawahimiza wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili waweze kuwania nafasi hizo.
Boniface Wambura

     MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI TASWA

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.