Monday, February 24, 2014

TIGO YAWEKA HISTORIA NYINGINE YA DUNIA,SASA UNAWEZA KUTUMA PESA KWA TIGO PESA UKIWA RWANDA NA TANZANIA,HABARI NZIMA IKO HAPA

MAMBO YA TIGO
BALOZI WA RWANDA BEN RUGANGAZA AKIWASILIANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA WAKATI AKIMTUMIA HELA KWA TIGO PESA KWA MARA YA KWANA KATIKA HUDUMA HIYO AMBAYO IMEZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM NA MUDA HUOHUO IKIZINDULIWA NCHINI RWANDA

            Kampuni ya mawasiliano ya TIGO TANZANIA leo imeweka historia nyingine ya dunia baada ya kuzindua huduma yake mpya ambayo sasa unaweza kutuma na kupokea pesa  ukiwa nchini Rwanda na Tanzania kwa kutumia tigo pesa kwa Tanzania na tigo cash kwa Rwanda

    Huduma hiyo ambayo imezinduliwa leo katika tafrija mbili tofauti moja ikiwa Tanzania na nyingine ikiwa Rwanda inatajwa kuwa ya kwanza kufanyika duniani kwani katika huduma hiyo  unaweza kupokea pesa za nchi husika kama zilivyotumwa

    Huduma hiyo ilishuhudiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania bw BEN RUGANGAZA pamoja na balozi wa Tanzania nchini Rwanda,ambapo wote kwa pamoja wameipongeza kampuni ya tigo kwa kufanikisha huduma hiyo ambayo inatajwa kuwa ya kwanza kutokea Tanzania na duniani kwa ujumla.

      Kwa mujibu wa mkurugenzi wa tigo Tanzania DIEGO GUTIEREZ amesema kuwa baada ya mteja kupokea pesa ikitokea baina ya nchi hizo mbili mteja anaweza kuitumia kulipia huduma zote za tigo zinazopatikana katika tigo pesa au tigo cash kwa Rwanda.

      Amesema kuwa huduma hii itaokoa muda mwingi sana ambao wateja wake wanchi hizo mbli walikuwa wanaupoteza katika kutuma pesa huku akitaja jinsi ya kuipata huduma hiyo kuwa ni *150*90#  ka Tanzania huku wale walioko Rwanda wakipiga *200*7#.

MKURUGENZI WA TIGOTANZANIA BW DIEGO GUTIERREZ AAKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO LEO


No comments: