Add caption |
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita Tangu
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba kutoa Msimamo
kuhusu muundo wa Serikali Tatu hauepukiki kwenye Bunge maalum ya Katiba nchini,Chama
Cha Mapinduzi CCM kimeibuka na Kumsuta mwenyekiti huyo
Na kusema kamwe chama hicho akiwezi kuunga
mkono serikali tatu badala yake chama hicho kitashikilia msimamo wake wa Muundo
wa Serikali mbili.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar
es Salaam na Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi ya Chama
hicho,Nape Mosses Nnauya wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ambapo
alisema CCM hawawezi kuunga mkono muundo wa watu wachache wa serikali tatu.
“Bado CCM inaamini changamoto
za muungano huu ni Suluhisho lake
sio kubadili muundo wa
muungano tulionao bali ni kuufanyia maboresho muundo tulionano wa serikali
mbili,hivyo basi bado CCM inaamini muundo bora kwa sasa utakaodumisha muungano
wetu ni SERIKALI MBILI”alisema Nape
Nape aliongeza na kusema
chama hicho kinazidi kusimamia misimamo
yake kamwe hawezi kuunga muundo wa
Serikali tatu kwani ni muundo wa watu wachache wasiokuwa na maslai kwa muungano
wetu.
“Kimsingi CCM ndio waasisi wa
Muungano huu wa Tanganyika
na Zanzibar.CCM Ina maslai makubwa na mapana na muungano huu kama
waasisi pengine kuliko taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu”aliongeza Nape
Vilevile Chama hicho
kimewaomba wananchi kutokubali muundo wa serikali tatu na badala yake kuwa watulivu katika kipindi hiki
na kusubili hatua zilizobaki katika Mchakato huu wa kupata katiba mpya.
“CCM inaamini awamu mbili zilizobaki
kwa kuwa zinahusisha
wakilishi wa wananchi kupitia
Bunge maalum la katiba, na Hatimaye itawahusisha wananchi wenyewe moja kwa moja
kupitia kura yao
Zitumike vizuli kutupa kutupa Katiba ”aliongeza Nape
No comments:
Post a Comment