Saturday, March 22, 2014

EXCLUSIVE---JUMAMOSI SIO NZURI HUKO TABATA--MOTO WATEKETEZA NYUMBA MOJA TABATA KIMANGA ASUBUHI YA LEO,CHEKI PICHA ZOTE ZA TUKIO HILO,WANANCHI WATUPA LAWAMA KWA WATU WA ZIMAMOTO KWA KUCHELEWA

Muonekano wa nyumba hiyo kwa nje meneo ya tabata kimanga ambayo majira ya asubuhi leo imetekea kwa moto yote huku wananchi wakilalamikia uchelewaji wa zimamoto ambao wamefika tayari asilimia kubwa ya nyumba hiyo imekwisha teketea


Moto ukiwa tayari umesambaa eneo lote la nyumba hiyo

Hao ndio zimamoto wakiwasili kwa kuchelewa zaidi ya masaa mawili tangu moto uanze ambapo hata hivyo hawajafanikiwa kuokoa kitu cha maana
Moto mkubwa wateketeza nyumba leo maeneo ya Tabata kimanga jijini Dar es Salaam,moto huo iliyotokea  mnamo majira ya saa moja na nusu asubuhi katika nyumba ya bibi na bwana Ngonyali ilisababishwa na itilafu ya umeme ambapo babu mwenye nyumba hiyo alikuwa amekwenda Jumuiya na bibi akiwa shamba bagamoyo
mtoto Ogi Paul mwenye umri wa miaka (7) mjukuu alikuwa amelala katika chumba ulipoanzia moto huo,na msichana mdogo wa kazi katika nyumba hiyo.

Mwenye nyumba akigombana bada ya kutokea ugomvi mkubwa katika eneo hilo
Fire wakifanya yao



chanzo rasmi cha moto huo hakijafahamika huku baadhi ya wahusika wa nyumba hiyo kila mmoja akisema lake,kuwa ni hitilafu  ya umeme nae msichana wa kazi wa nyumba hiyo akisema mjukuu aitwae Ogi Paul alikuwa akichezea mshumaa wakati akiwa katika kitandani ndio ukashika katika godoro.
Saa mbili na dakika 24 ndio faya wamefika eneo la tukio baada ya kupigiwa simu tangu saa moja asubuhi,Ambapo mzee Ngonyali aliwazuia kwenda kuzima akisema’’rudini mlipotoka hamna faida,mnakuja kuokoa nini na kila kitu kimeshateketea?rudini nimesema sitaki kuwaona’’ kabla ya baadhi ya wakazi wa mtaa huo kuwasihi zimamoto hao kuja kumalizia kuuzima moto huo.
Moto huo ulifanikiwa kuzimwa Saa tatu na dakika 20


Baada ya muda TANESCO wakawasili na hapa wakaamua kukata umeme kuepuka matatizo mengine zaidi

TANESCO

Wananchi wakiwabembeleza watu wa zimzmoto kurudi katika eneo la tukio baada ya kutaka kuondoka kutokana na ugomvi mkubwa uliotokea
Nae mkazi wa eneo hilo aliejitambulisha kwa jina moja la Alex amesema upo umuhimu wa kuwa na gari ya zima moto kila kata ili kupunguza hasara kama hii iliyotokea sababu watu wa zima moto hawana desturi ya kufika kwa wakati maeneo ya matukio ya moto---SHUKRANI ZA PEKEE ZIENDE KWA MWANDISHI WETU FATMA JALALA KWA KUFANIKISHA HABARI HII

No comments: