HII NDIO HABARI INAYOTIKISA JIJI KWA SASA---ASKARI WANNE (4) WA JESHI LA POLISI WAFUKUZWA KAZI KWA FEDHEHA KWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHALIFU

kamishna wa kanda maalum ya dar es salaam suleman kova akizungumza na wanahabari muda huu ofisini kwake juu ya kufukuzwa kwa askari hao.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewafukuza kazi kwa fedheha askari wanne wa Jeshi la Polisi kutokana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu. Askari waliofukuzwa wanatoka katika vikosi mbalimbali kama ifuatavyo:
·        
E.6396 CPL RAJABU MKWENDA @ UGORO wa Makao Makuu ya Polisi.
·       F.9412 PC SIMON wa Kituo cha Polisi Kati.
·       F.9414 PC ALBERNUS  KOOSA wa Kikosi cha Bendi ya Polisi D’Salaam
·       F.9512 PC SELEMAN wa Kituo cha Polisi Kigamboni
Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba askari hao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu ikiwa ni pamoja na tukio la tarehe 09/03/2014 eneo la Mbezi Beach “A” ambapo majambazi wapatao  15 walifika katika ofisi ya Kampuni ya Kichina ijulikanayo kwa jina la HONG 

YANG inayojishughulisha na ujenzi na uselemala.
Katika tukio hilo majambazi wapatao 11 wakivamia ofisi hiyo majira ya saa 04:30 Asb, na kupora vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslim, simu, n.k. na kutoweka.

Imegundulika kwamba baadhi ya majambazi hai ni askari Polisi. Uchunguzi wa kina  umefanyika na watuhumiwa hao 11 wamepatikana ndipo ilipobainika kwamba askari Polisi hao walishiriki katika tukio hilo.
Watuhumiwa wengine saba wa ujambazi waliokamatwa ni hawa wafuatao:
·       GERADI S/O RAJABU MTUTU, Miaka 36, Mfanya biashara, mkazi wa Mtoni Mtongani.
·       CHARLES S/O HIZA MBELWA, Miaka 37, Fundi magari, Mkazi wa Kurasini.
·       ADAM S/O MKOMBIZI MOHAMED, Miaka 40, Mkazi wa Kariakoo.
·       ALLY S/O RASHID SALUM, Miaka 38, Mkazi wa Vingunguti Spenco.
·       SALUM S/O ABDUL MUSSA, Miaka 22, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbagala Kuu.
·       JUMA S/O SAID HAMIS, Miaka 29, Mkazi wa Yombo kwa Limboa.

·       JUMA S/O OMARI NGWELE, Miaka 50, Mfanyabiashara Samaki Ferry, Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.

Watuhumiwa wote hao wametambuliwa na mashahidi mbalimbambali katika tukio hilo. Kabla ya kufukuzwa kazi, askari hao walishtakiwa katika mahakama ya kijeshi na walipatikana na hatia hivyo wamepewa adhabu ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kulifedhehesha Jeshi la Polisi. wamefukuzwa kazi kuanzia tarehe 17/03/2014 na sasa si askari tena bali ni raia wa kawaida.
Aidha jalada la kesi hiyo pamoja na majalada mengine ya kesi ya wenzao waliowataja yatapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali hivi karibuni kabla ya kuwafikisha mahakamani kwa makosa jinai.
Pamoja na malezo hayo, Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Jeshi la Polisi na hatua hizi ni fundisho kwa askari wa cheo chochote atakayejaribu kwenda kinyume cha taratibu na maadili ya kazi.
Jeshi la Polisi litaendelea kuwazawadia askari wenye kufanya vitendo vya ujasiri vinavyoendena na tabia njema kama ilivyofanyika hivi karibuni tarehe 07/03/2014. Pia Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu maafisa, wakaguzi na askari watakaokiuka maadili au kukiuka mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi (Good Conduct)


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.