WAKILI ANNA HENGA AKIZUNGUMZA LEO |
Kituo
cha sheria na haki za binadamu Tanzania LHRC leo kimewataka wajumbe wa katiba
wa bunge la katiba kuweka kando maslah yao binafsi na badala yake kutanguliza
taifa mbele kwa lengo la kupata katiba iliyo bora na isiyobeba upande wowote.
Hayo
yamesemwa leo jijini dare s salaam na mkuu wa dawati la katiba la kituo hicho ANNA
HENGA wakatia akiwasilisha report iliyoandaliwa na kituo hicho kuhusu mwenendo
wa bunge hilo tangu lianze hadi sasa,ambapo amesema kuwa ni lazima wajumbe hao
kuweka kando itikadi zao za vyama vya kisisa na kuwatanguliza watanzania mbele
ili kuwapatia katiba iliyo bora kwa Tanzania ya sasa na ya baadae
Amesema
kuwa wao kama kituo cha sheria na haki za binadamu hawategemei kuona uchama,udini,ukabila
wala ukanda ukitawala katika bunge hilo
japo dalili za uchama zimeanza kuonekana kwa mbali na kukemea vikali tabia ya
watu kuonyesha misimamo ya vyama vyao katika maswala mbalimbali yanayowahusu
watanzania wote.
Aidha
akizungumzia swala la muda ambao wabunge hao watautumia kutengeneza katiba mpya
ambao umekuwa ukileta mkanganyiko amesema kuwa kwa mujibu wa kanuni ambazo
bunge hilo limejiwekea mapema wiki jana mwenyekiti anapewa nafasi ya kuongeza muda
pasipo na kikomo tofauti na ule uliowekwa wa siku 70 jambo ambalo amesema kuwa
ni hatari kuwa bunge linaweza kukaa hata miaka 3 huku likitumia mali za
watanzania bila sababu ya msingi.
No comments:
Post a Comment