makamu mk wa jukwaa la katiba tanzania hebron mwakagenda akizungumza leo
Jukwaa
la katiba tanzania JUKATA leo limetoa tahadhari kubwa kwa wabunge wa bunge
maalum la katiba Tanzania kwa kuwataka kuiheshimu rasimu ya katiba mpya ambayo
ndio wanaijadili bungeni badala ya kuibeza na kuiona kama haina maana.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam
na makamu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania bw HEBRON MWAKAGENDA wakati
akizungumza na wanahabari leo ofisi za jukwaa hilo na kusema kuwa kazi
iliyofanyika na tume ya katiba Tanzania ni kubwa sana na haifai kubezwa hata
kidogo huku wakimpongeza mwenyekiti wa tume hiyo jaji JOSEPH WARIOBA .
Bw MWAKAGENDA amesema kuwa hata Raisi wanchi
hana budi kuiheshimu rasimu hiyo kwani hayo ni maoni ya watanzania walio wengi
hivyo hana budi kwaachia wajumbe hao waijadili kwa uhuru.
Aidha katika hatua nyingine jukwaa
la katiba Tanzania limekemea vikali vitendo vya
vurugu vilivyoanza kujionyesha bungeni hapo huku kukiwa na zome zomea ya
wabunge na vurugu za kila siku ambapo wamesema kuwa vitendo hivyo haviwapendezi
watanzania ambao wanasubiri katiba mpya hivyo kuushauri uongoizi wa bunge hilo
kuwa makini kwa kuwachukulia hatua kali wale wote ambao wanafanya vitendo
hivyo.
|
No comments:
Post a Comment