WAUZA UNGA HAWAISHIWI MBINU MPYA,POLISI YAKAMATA WANNE WAKIWA WAMEFICHA UNGA KWA STAILI YAKE,JIONEE HAPA,KAMISHNA KOVA ASEMA AMEWASHTUKIA SASA WAMEKWISHA

Kamishna kova akizungumza na wanahabari mchana wa leo kuhusu tukio hilo ambapo mnamo tarehe 18 mwezi wa tatu mwaka huu majira ya saa nane mchana watu wanne ambao watatu  kati yao ni wanaume raia wa nigeria na mmoja wa kike raia wa tanzania walikamatwa na kifurushi wakijiandaa kusafirisha dawa za kulevya aina ya herion na cocein kwenda nchini liberia ambapo dawa hizo zilikuwa zimewekwa kwenye vitabu mbalimbali vya shule kama utakavyojionea katika picha wakijifanya wanasafirisha vitabu
Ukiona utadhani ni kitabu kwa ajili ya kusomea kumbe ni kwaajili ya kufanyia uhalifu huu,mbinu hii imeanza kutumika sasa na wahalifu wa madawa ya kulevya ambapo kamanda kova amesema jeshi la polisi tayari limetambua mbinu hiyo na tayari wameanza kuifanyia kazi kuhakikisha haifanukiwi

Madawa ya kulevya maarufu kama unga ambayo jeshi la polisi kanda maalum ya dar es salaam wamefanikiwa kuyakamata yakiwa yamewekwa kwenye vitabu huku waalifu hao wakijifanya kuwa wamebeba vitabu kumbe ni uhalifu mkubwa
Hivi ndivyo unga huo unavyopachikwa katikati ya kitabu na kisha kufunikwa vizuri kabisa

Katikati ya kitabu ndiko kunakofishwa unga huo na kujifanya kama wamebeba shehena ya vitabu kumbe ni madaw ya kulevya
Kamanda kova amewataja kwa majina wahalifu hao kuwa ni SUNDAY NNABUFEE CHAIKAOBI ambaye ni mnigeria  mkazi wa kimara,CHKWUMA EHN FAVOUR raia wa nigeria mkazi wa buguruni,FRANKILIN ANOCHIL na KHADIJA JUMANNE NGOMA mkazi wa kimara

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.